Tuesday, August 6, 2024

BALAOZI WA SWEDEN NCHINI TANZANIA ATEMBELEA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI KILIMANJARO

Agosti 05, 2024 Balozi wa Sweeden nchini Tanzania Mh. Charlotta Ozaki Macias ametembelea Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na klabu hiyo pamoja na kufanya mazungumzo na wanachama wa mkoa huo.

Mh. Balozi huyo pia ametaka kujua mchango wa MECKI kwa jamii katika kupaza sauti ili kuibua changamoto zilizopo kwenye jamii na namna klabu hiyo ilivyojipanga kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa 2025.

Pamoja na mambo mengine Balozi na wanachama hao wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na namna ya kuandika habari za uchaguzi.

Pia Charlotta ameambatana na timu kutoka Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) iliyokuwa ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Kenneth Simbaya.


No comments:

Post a Comment