Wednesday, August 7, 2024

MADIWANI WAKOSHWA NA UTENDAJI WA KAZI WA DED RUNGWE

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya wameridhishwa na utendaji kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Renatus Mchau na kukubaliana shule mpya ya ufundi  inayotarajiwa kujengwa kuitwa jina la mkurugenzi huyo kama sehemu ya kuenzi mchango wake wa kusimamia na kukuza elimu kupitia utendaji wake ulioleta matokeo yenye tija.

Madiwani wamefikia makubaliano hayo baada ya kujiridhisha na mabadiliko yaliyoletwa na Mkurugenzi huyo ikiwemo kuongezeka ufaulu wa shule za Sekondari na kumaliza tatizo la vifo vya mama na mtoto katika Halmashauri hiyo kwa muda wa miezi saba.

"Haijawahi kutokea halmashauri hii kutokuwepo watoto wenye zero, lakini Sasa hivi wanafunzi wamefaulu daraja la kwanza na la pili shule zote za Sekondari, huyu Mkurugenzi ameleta Mapinduzi makubwa sana lazima aache alama kwenye wilaya yetu, maana ni mfano wa kuigwa".

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Renetus Mchau amewataka watumishi kuwa waadilifu ili waweze kutoa huduma kwa weredi na kuzingatia kanuni za utumishi hali itakayochochea matokeo chanya.


No comments:

Post a Comment