Monday, August 26, 2024

FYANDOMO: DKT. SAMIA AMETATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI MBEYA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo amesema kitendo cha Rais Samia Suluhu Hassan kuleta fedha za miradi ya Maendeleo amelenga kutatua kero za wananchi hususan katika sekta ya afya na Maji.

Fyandomo amesema leo Jijini Mbeya baada ya kushiriki mbio za Mwenye wa Uhuru Kitaifa 2024  akiwa   amewawakilisha Wabunge wa Mkoa wa Mbeya.

Amesema kikubwa wanaendelea kuishukuru serikali kupitia  Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson kuwasilisha kero za wananchi.

"Kama mwakilishi wa wabunge nishukuru serikali na viongozi wa mbio za mwenge kwa kuja kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Mbeya" amesema.

Amesema kama wabunge wataendelea kushirikiana na serikali hususan kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya kutatua kero za wananchi katika maeneo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment