Tuesday, August 6, 2024

TIRA WAJA NA MIKAKATI UHAMASISAJI BIMA YA AFYA, KILIMO

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imekuja na mikakati ya uhamasishaji wakuu wa mikoa na wilaya kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na umuhimu wa kukata bima za afya majanga ya moto na sekta ya kilimo katika uzalishaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Agosti 6, 2024 Kamishna wa Bima nchini, Baghayo Saqware amesema lengo la kukutana na wakuu wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuhamasisha kuhusiana na utekelezaji wa sheria ya bima ya afya kwa wote.

Mbali na hilo pia kutambulisha ofisi za Kanda na majukumu ya Mamlaka hiyo kwa ili waweze kuwa mabalozi kwa wananchi wanao wasimamia kutumia bidhaa za bima.

Naye Mkuu wake Mkoa wa Mbeya Juma Homera amewataka watendaji wa TIRA kuongeza wigo mpaka kufika maeneo ya vijiji kutoa elimu ya umuhimu wa bima za afya na mashamba.

Amesema wananchi wakipata elimu watakua chachu ya kutumia bidhaa za bima kwa lengo la kuepukana na majanga mbalimbali ya ikiwepo moto na ajali,majengo na mashamba.

"Kama Wakuu wa Mikoa tutashirikiana na TIRA kuona tunawafikia wananchi na kuwapatia elimu ili kufikia malengo ya serikali katika uwekezaji kwenye sekta ya afya nchini" amesema.

Naye Meneja wa Kanda Neema Lutula amesema wataendelea kuhamasisha jamii kuwa na bima ambazo ni msaada mkubwa katika masuala ya afya na sekta ya kilimo kwenye uzalishaji.

No comments:

Post a Comment