Thursday, August 8, 2024

WANANCHI KALOBE MWAKIBETE, WAMPONGEZA DKT. TULIA KWA KUONGEZA MIRADI MBEYA

Wananchi wa kata ya Kalobe na Mwakibete Jijini hapa wamesema kuna kila sababu ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson kwa ujio wa miradi mingi ya kimkakati yenye tija kwao.

Wakizungumza na Mwandishi wa wahabari kwa nyakati tofauti wamesema kwa kupindi cha miaka mitatu Dkt. Tulia na Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza serikali ya awamu ya sita wameona mageuzi makubwa katika nyanja mbalimbali kama elimu, afya maji na miundombinu ya barabara.

Joyce Aloyce mkazi wa Shewa Jijini hapa amesema jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mwakibete na kwamba wana deni katika uchaguzi Mkuu 2025.

"Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita tulikuwa gizani lakini baada ya kutoka usingizini na kurejea CCM tunaona upatikanaji wa huduma muhimu za maendeleo kama maji, miundombinu ya barabara, afya, elimu ikitekelezwa kwa vitendo" amesema.

Naye mkazi wa Kalobe Thobias Mwakyusa amesema hali ya wananchi mitaani imekuwa na unafuu sambamba na kuondolewa kwa michango ya madawati mashuleni.

Amesema miaka kadhaa iliyopita walikuwa hawalali kutokana na watoto kufukuzwa mashuleni kwa  kukosa michango hususani ya madawati,matundu ya vyoo na hata kukaa sakafuni.

"Dkt. Tulia Mwanamke aliyemzaa alikuwa na utulivu ni watu wachache wanaogusa jamii yenye kipato duni tumeshuhudia matibabu macho, vitimwendo, ujenzi wa makazi, utoaji wa bima za afya na sare kwa wanafunzi mazingira  magumu" amesema.

Thobias amesema mbali na mafanikio hayo wanaomba serikali   kuboresha barabara za mitaa ili kuondoa vumbi .

Akijibu hoja hizo za wananchi Mbunge wa Mbeya mjini,Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson amesema serikali ya awamu ya sita imekuja na mpango wa kujenga barabara za mitaa hivyo wananchi wasiwe na shaka.

"Niwatoe hofu Waziri wa Tamisem Mohamed Mchengerwa alikuja kushuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara za mitaa,stendi kuu ya mabasi ya mikoani na Soko la kisasa la matola" amesema.

Amewataka wananchi wasiwe na shaka watarejea kusuka nywere na kupendeza huku akieleza uwepo wa vumbi kwenye barabara za mitaa zinapalekea wakinamama kushindwa kusuka nywele nzuri.

Dkt. Tulia amesema mbali na miradi hiyo pia serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza katika ujenzi wa shule za sekondari, msingi sambamba na ukarabati wa shule kongwe ili kuwezesha watoto kusoma katika mazingira salama.

Kuhusu suala la maji amesema mradi wa kimkakati wa mto kiwira umakuja kuwa suruhisho la kudumu la tatizo la mgao wa maji huku akitahadharisha wananchi kutunza maji kufuatia kuwepo kwa mgao wa maji kipindi hiki cha kiangazi.

No comments:

Post a Comment