Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambae pia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, amefika Jimboni kwake na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa huku pamoja na mambo mengine wamejadili kuhusu namna bora ya kuboresha Maendeleo ya Jiji la Mbeya katika sekta mbalimbali.
Wakati huo huo Dkt. Tulia anatarajia kufanya zoezi la kugawa bima za afya bure kwa kaya 600 za jijini hapa.
No comments:
Post a Comment