Saturday, February 24, 2024

KAMPUNI YA PCT YATOA MSAADA WA MIFUKO 30 YA SARUJI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI


Kampuni ya Pareto PCT imetoa msaada wa mifuko 30 ya saruji kwa Shule ya Sekondari Mwakipesile, Shule mbili shikizi katika vijiji vya   Iswago Ruanda.

Kati ya mifuko hiyo 30 mifuko 10 imeelezw kutumika kwa ajili ya  ambayo itatumika kwa  ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu na miundombinu ya vyumba vya madarasa.

Msaada huu umetolewa na Kampuni ya PCT kupitia Afisa Pareto wa Mikoa ya Mbeya na Songwe, Mussa Malubalo.

Kwa upande wake Afisa pareto, amewashukru wakulima wa vijiji vya Iyunga Mapinduzi, Iswago na Ruanda kwa kuendelea kuiamini kampuni hiyo kuendelea kuiuzia maua.


Aidha amewataka na kuwasisitiza wasichoke kuuza maua PCT na wao hawatachoka kuwasaidia wakulima na kurudisha msaada kwa jamiii ili gurudumu la maendeleo liweze kusonga mbele.

Pia Kampuni ya PCT haijaishia kwenye kutoa msaada wa saruji  bali kipindi hiki cha mvua nyingi wameweza kutoa (booster fertiliser) mbolea ya maji kwa ajili ya kukuza na kukinga miche inayoungua kwenye vitalu kwa mvua nyingi.

Pia wanaendelea na zoezi la kugawa miche ya zamani (Makomoni) kwa wakulima ambao wameunguliwa na miche yao kwenye vitalu.

No comments:

Post a Comment