Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, amezindua na kumkabidhi nyumba mlemavu wa macho Hosea Kalemale Mkazi wa Kata ya Mwakibete Jijini.
Makabidhiano hayo yamefanyika Februari 23, 2024 huku mamia ya wananchi wamejitokeza kushuhudia huku wengine wakimuombea Dk Tulia Mungu ampe maisha marefu kwa kitendo cha kijitoa kusaidia wahitaji.
Dkt. Tulia amemkabidhi Hosea nyumba hiyo yenye vyumba viwili vya kulala, sebule pamoja na choo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa siku kadhaa mara baada ya kuombwa hitaji hilo.
“Sitaishia hapa, hata nikifikia hatua ya kuachana na masuala ya kisiasa sitaacha kusaidia watanzania na sio kwamba sasa naacha siasa hapaka ukifika wakati” amefafanua.
Kwa upande wake, Chifu wa Mkoa wa Mbeya, Rocket Mwashinga amesema watamlinda Dk Tulia popote aendapo kwani ni tunu ya Mkoa wa Mbeya.
“Tutamlinda tunavyojua sisi hatadhurika kwani amekuaa mstari wa mbele kuleta Maendeleo ya wanambeya na kwamba Mbeya imetulia na Dkt. Tulia Ackson” amesema.
Diwani kata ya Mwakibete, Lucas Mwampiki amesema kuwa mwaka 2025 hakuna mtu wa kuchukua fomu kugombea nafasi ya ubunge na Urais wananchi wana deni kubwa .
“Dkt. Tulia hatuelewi tuseme nini naishiwa maneno ya kusema umekuwa na mchango mkubwa sana kwa jamii na hata kusukuma miradi ya maendeleo katika nyanja za elimu afya na miundombinu ya barabara na maji ” amesema.
Akitoa Neno la Shukrani Mnufaika wa nyumba hiyo, Hosea amesema kuna kila sababu watanzania kumuunga mkono Dkt. Tulia kwani anawagusa hata wanyonge kama yeye.
“Nikuombee Mungu aendelee kukupandisha nafasi ya Juu kwa Taifa la Tanzania kwani umeshika nyadhifa kubwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na bado unatusaisia wananchi wa chini na Mimi leo nimejaza watu wengine walikuwa hawakujui” amesema.
Wakati huo huo ameomba mtaji kwa ajili ya kuuza banda la vinywaji baridi katika eneo la Kabwe na mradi wa pikipiki ya matairi matatu (Bajaj) ambayo ameona ni ndoto yake itakayomuinua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment