Thursday, February 15, 2024

TAASISI YA TULIA TRUST YAJA NA MIKAKATI YA KUIHUDUMIA JAMII YA JIJI LA MBEYA 2024.

 Tasisisi ya Tulia Trust ambayo Mkurugenzi wake ni Spika wa Bunge, Mbunge wa Mbeya mjini na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) imekuja na mipango kabambe ya kuhudumia jamii ya Jiji la Mbeya huku ikianza kufanya  mazungumzo na  wa Serikali ikiwepo Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya na Mstahiki Meya Dormohamed Issa.

Hatua hiyo imeanza kwa mazungumzo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa nyakati tofauti ambapo jana a Februari 13, 2024 wamefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, John Nchimbi na Leo Jumatano Februari 14, 2024 wamefika Ofisi ya Mstahiki Meya Dormohamed Issa .

Wakati huo huo wameweza kueleza pia mipango yao kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Malisa kuhusiana na mikakati hiyo Taasisi kuigusa jamii kwa mwaka 2024.

Mbali na mazungumzo hayo pia wamepata fursa ya kutoa fulana (T- shart )  maalumu zenye ujumbe  mahususa wa wa Taasisi ya Tulia Trust na Rais Samia Suluhu Hassan 'Tumetulia na Rais Samia' ukisomeka hivyo.

Kiongozi wa msafara huo Meneja wa Taasisi ya Tulia Trust, Jackline Boaz amesema lengo ni  kufanya  mazungumzo kuhusu namna taasisi tunavyo fanya kazi ya kuhudumia jamii, kuendelea kuimarisha mashirikiano na za Serikali.

Pia ni  kuelekeza mikakati tuliyo nayo kwa mwaka 2024 ya kuhakikisha tunaihudumia jamii ya Jiji la Mbeya kikamilifu katika kuunga mkono Juhudi za Spika wa Bunge ambaye ni Mbunge wa Mbeya mjini, Dkt. Tulia Ackson ambaye pia nia Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Kwa upande wake Mstahiki Meya Jiji la Mbeya, Dormohamed Issa amesema Jiji la Mbeya wamajivunia uwepo wa Rais wa IPU, Dk Tulia na kwamba amekuwa ni Connection ya kulifanya jiji la Mbeya kupiga hatua za maendeleo.

“Jiji la Mbeya tunajivunia na kutembea kifua mbele kwa sababu ya Dkt. Tulia kwa kweli tunafanya maendeleo ya kasi ya ajabu katika nyanja za elimu, afya miundombinu ya barabara njia nne sambamba na  mradi mkubwa wa maji kutoka mto Kiwira” amesema.

Amesema kama Jiji wanahaidi kushirikiana na Taasisis hiyo katika kuhakikisha wananchi wa Mbeya wanafikiwa na huduma kwa wakati sambamba na kushiriki katika matukio mbalimbali yatakayoratibiwa na Taasisi hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya, Beno Malisa amesema kama Serikali wataendelea kuunga mkono Taasisi hiyo kwani imekuwa na mchango mkubwa sana kwa wananchi wa Wilaya ya Mbeya na Jiji kwa ujumla

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust, Joshua Mwakanolo amesema wanaendelea kuishika jamii yenye uhitaji wakiwepo wazee,yatima na wenye mahitaji katika Jiji la Mbeya hususan kuwa na mipango kabambe kwa mwaka 2024.

No comments:

Post a Comment