Monday, August 26, 2024

MEYA ISSA: DKT. TULIA MBUNGE MAKINI, MAHIRI KULETA MAENDELEO MBEYA

Mstahiki Meya Jiji la Mbeya Dourmohamed Issa, amesema umahili wa Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson ameleta mabadiliko makubwa kwa Jiji la Mbeya katika kuleta maendeleo ya miradi ya kimkakati.

Issa amesema mara baada ya kushiriki mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa 2024 wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye  mradi wa Maji Itagano - Mwanswekwa wenye thamani ya Sh 5 bilioni wenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni mbili kwa siku.

Amesema Dkt. Tulia ni Mbunge wa kitofauti kwa mahiri na umakini na amekuwa anafikika namna ya kulipambania jimbo la Mbeya kuleta maendeleo ikiwepo utekelezaji wa mradi huo wa Maji ambao utakuwa na tija kubwa kwa wananchi.

FYANDOMO: DKT. SAMIA AMETATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI MBEYA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo amesema kitendo cha Rais Samia Suluhu Hassan kuleta fedha za miradi ya Maendeleo amelenga kutatua kero za wananchi hususan katika sekta ya afya na Maji.

Fyandomo amesema leo Jijini Mbeya baada ya kushiriki mbio za Mwenye wa Uhuru Kitaifa 2024  akiwa   amewawakilisha Wabunge wa Mkoa wa Mbeya.

Amesema kikubwa wanaendelea kuishukuru serikali kupitia  Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson kuwasilisha kero za wananchi.

"Kama mwakilishi wa wabunge nishukuru serikali na viongozi wa mbio za mwenge kwa kuja kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Mbeya" amesema.

Amesema kama wabunge wataendelea kushirikiana na serikali hususan kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya kutatua kero za wananchi katika maeneo mbalimbali.

THRDC YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI

Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali, (kushoto Frolian Godwin kutoka Mwanza, Kenneth Ngelesi Kutoka Mbeya na Ediga Rwenduru kutoka Geita) wakiwa katika picha ya pamoja baada kushiriki mafunzo ya jinsi ya kuripoti habari za uchaguzi iliyofanyika Jijini Dodoma kwa siku mbili chini ya uratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC.


Friday, August 16, 2024

WALIOHITIMU ELIMU YA KIDATO CHA SITA KWA UFADHIRI WA DKT. TULIA NIGERIA WAWASILI NCHINI

Wanafunzi  watano waliokuwa wakisoma nchini Nigeria kwa ufadhiri wa Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wa Spika wa Bunge Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wamewasili leo Ijumaa Agost 16 mwaka huu.

Mapokezi hayo yamefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Songwe huku ndugu jamaa na viongozi mbalimbali walishiriki wakiongozwa na Meneja wa Taasisi ya Tulia Trust Jackline Boaz.

Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo Jackline amesema vijana hao watano akiwepo wa kiume mmoja walikuwa wakiishi katika mazingira magumu na kwamba walipata ufadhiri kuanzia kidato cha kwanza mpaka sita katika moja ya shule nchini Nigeria.

MKANDARASI WA MRADI MTO KIWIRA ATAKIWA KUONGEZA KASI

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amemtaka mhandisi mshauri wa Kampuni ya  GKW Consult GmbH kuharakisha ujenzi wa usanifu wa chanzo cha Maji Mto Kiwira Wilaya ya Rungwe kabla ya msimu wa kifuku kuanza.

Mhandisi Mwajuma amesema leo Mkoa wa Mbeya katika ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa chanzo cha Mto Kiwira na tenki la Maji katika eneo la New Forest.

Amesema mhandisi mshauri anapaswa kuongeza nguvu ya ujenzi ili kwenda na kasi mvua zikianza watashindwa kutekeleza na kukamilika ifikapo Aprili 2025 kama makubaliano ya mkataba ulivyosainiwa.

Wednesday, August 14, 2024

"JIJI WEKENI MFUMO MZURI WA BAJAJI KUSHUSHA ABIRIA STENDI KUU" MWASELELA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (NEC) Mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela  ameutaka uongozi wa halmashauri ya Jiji kuweka mfumo mzuri wa ulipaji wa ushuru wa madereva bajaji na kuwaruhusu kushusha abiria stend kuu ya mabasi ya mikoani.

Mwaselela amesema leo Agosti 14 mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku ya tatu tangu akutane na madereva wa bajaji jiji la Mbeya zaidi ya 2,000 kwa lengo la kusikiliza kero zao.

Amesema miongoni mwa kero alizopokea na kuzitolea majibu  ni pamoja na  bajaji kuzuiwa kuingia kushusha abiria ndani ya stendi kuu hali  hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria .

"Kuna eneo ambalo wametengewa lakini wamelalamikia sio rafiki ambalo sambamba na sehemu za maegesho ambayo itakuwa na maelekezo ili waweze kulipia" amesema.

Tuesday, August 13, 2024

1,000 KUSHIRIKI MASHINDANO YA MAPISHI

 

Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi Wake ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson imeandaa Mashindano ya Mapishi kwa Mama na Baba Lishe  Mbeya Mjini.

Mashindano hayo yanajulikana kama  Tulia Cooking Festival yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi Agosti  2024 na  yakishirikisha washiriki 1,000 yenye kauli mbiu isemayo tumia nishati mbadala kuondoa uchafuzi wa mazingira.

Taasisi ya Tulia Trust imekuwa ikifanya matamasha mbalimbali kwa ajili ya kuwapa fursa mbalimbali watanzania ikiwa ni pamoja na kuwainua kiuchumi.


Monday, August 12, 2024

DKT. NCHIMBI AAGIZA VIONGOZI WA CHADEMA, WAANDISHI WA HABARI WAACHIWE HURU


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amemwagiza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Daniel Sillo kuzungumza na waziri wake, Hamad Masauni, kuwaachia huru viongozi wa Chadema waliokamatwa na Polisi mkoani Mbeya.

Dkt. Nchimbi amesema hayo leo Agosti 12, 2024 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Katoro iliyopo mkoani Geita anakoendelea na ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Amesema alifanya jitihada za kuwatafuta viongozi wenzake wa vyama vingine vya siasa, ili wawe na mazungumzo kama vyama vya siasa, aliwasiliana na baadhi ya makatibu wakuu, hata hivyo alipata taarifa wengine wamekamatwa mkoani Mbeya.

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUANDIKA HABARI ZA KUISAIDIA JAMII

Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuandika habari zitakazosaidia kutatua kero za wananchi kwa kuwa habari hizo zitasaidia kurejesha imani ya wananchi kwa vyombo vya habari.

Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC) Keneth Simbaya, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipozungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo.

Simbaya alisema kwa miaka ya karibuni imani ya wananchi kwenye vyombo vya habari imeshuka kutokana na waandishi wa habari kuripoti habari ambazo hazina tija kwao.


WANANCHI RUIWA NA MAHONGOLE WAOMBA KUTENGENEZEWA DARAJA LILILOHARIBIWA NA MAFURIKO

Wananchi wa Kata za Ruiwa na Mahongole Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wameiomba Serikali kuwajengea daraja jingine eneo la Msikitini linalounganisha Kata ya Ilongo, Ruiwa na Mahongole lililoharibiwa na mvua za elinino mapema mwaka huu.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema daraja hilo kwa sasa ni hatarishi kwa waendesha bodaboda ambao wametengeneza kiunganishi cha muda kwa kutumia mbao na kwa sasa halina uwezo wa kupitisha magari hivyo kufanya gharama kubwa za nauli.

Diwani wa Kata ya Ruiwa Kassim Mtale amesema kukatika kwa daraja hilo kumeongeza umbali wa kilometa tatu kutoka daraja hilo kufika Ilongo.

Friday, August 9, 2024

JIJI LAAGIZWA KUTOA HATI KWA WANANCHI WALIOKUMBWA NA MAPOROMOKO YA TOPE

Halmashauri ya Jiji la Mbeya imetakiwa kutoa hati miliki za viwanja kwa wathirika wa maporomoko ya tope la mlima Kawetere kata ya Itezi jijini hapa.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Agosti 9 mwaka huu mara baada ya Dkt. Tulia kufanya mkutano na waathirika hao kutatua mgogoro wa kujenga katika eneo walilopewa  viwanja kwa ajili ya makazi.

Sambamba na hilo Mbunge huyo na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) pia amekabidhi kitita cha Sh. milioni 25 zilizotolewa na Mwenyekiti Taifa wa Umoja wa Wanawake UWT Mary Chatanda.

Amesema awali baada ya kutokea maporomoko ya tope kutoka mlima Kawetere serikali ilitoa  maelekezo ya wananchi hao kupewa viwanja na sio kulipia hati miliki.

DKT. TULIA AWATOA HOFU WAFANYABIASHARA WA SOKO LA IGAWILO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wafanyabiashara wa Soko la Igawilo lilolopo Kata ya Igawilo Jijini Mbeya kuendelea kufanya shughuli zao kwa amani ili kujipatia vipato vyao.

Dkt. Tulia ameyasema hayo Agosti 8, 2024 wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea Wafanyabiashara wa soko hilo kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi ambapo miongoni mwa kero walizomtajia ni pamoja na ubovu wa miundombinu, tozo za Halmashauri pamoja na muingiliano baina ya Wafanyabiashara wa ndani na nje ya soko hilo ambapo amewahakikishia kuzitatua kwa kushirikiana na Serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Mhe. John Nchimbi, amesema kuwa Serikali imeanza kuzifanyia kazi changamoto za Wafanyabiashara hao na itahakikisha inazitatua kwa haraka. 

Thursday, August 8, 2024

WANANCHI KALOBE MWAKIBETE, WAMPONGEZA DKT. TULIA KWA KUONGEZA MIRADI MBEYA

Wananchi wa kata ya Kalobe na Mwakibete Jijini hapa wamesema kuna kila sababu ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson kwa ujio wa miradi mingi ya kimkakati yenye tija kwao.

Wakizungumza na Mwandishi wa wahabari kwa nyakati tofauti wamesema kwa kupindi cha miaka mitatu Dkt. Tulia na Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza serikali ya awamu ya sita wameona mageuzi makubwa katika nyanja mbalimbali kama elimu, afya maji na miundombinu ya barabara.

Joyce Aloyce mkazi wa Shewa Jijini hapa amesema jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mwakibete na kwamba wana deni katika uchaguzi Mkuu 2025.

"Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita tulikuwa gizani lakini baada ya kutoka usingizini na kurejea CCM tunaona upatikanaji wa huduma muhimu za maendeleo kama maji, miundombinu ya barabara, afya, elimu ikitekelezwa kwa vitendo" amesema.

Wednesday, August 7, 2024

BILIONI 117 KUTEKELEZA MRADI WA MAJI MTO KIWIRA, MBEYA

Serikali imetoa zaidi ya Sh Bilioni 117 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa kimkakati kutoka chanzo cha maji cha mto kiwira ambao unatarajia kukamilika Aprili 31 mwakani.

Mbunge wa Mbeya mjini  Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson amesema leo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi ya maji katika kata za Mwansekwa, Itagano na Ujenzi wa tenki kubwa  lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 70 kwa siku.

Dkt. Tulia amesema lengo la serikali ya awamu ya sita ni kutekeleza sera ya maji kwa vitendo sambamba na wananchi linapopita bomba la mradi wa mto Kiwira kunufaika na mradi huo ili kutunza miundombinu.


MADIWANI WAKOSHWA NA UTENDAJI WA KAZI WA DED RUNGWE

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya wameridhishwa na utendaji kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Renatus Mchau na kukubaliana shule mpya ya ufundi  inayotarajiwa kujengwa kuitwa jina la mkurugenzi huyo kama sehemu ya kuenzi mchango wake wa kusimamia na kukuza elimu kupitia utendaji wake ulioleta matokeo yenye tija.

Madiwani wamefikia makubaliano hayo baada ya kujiridhisha na mabadiliko yaliyoletwa na Mkurugenzi huyo ikiwemo kuongezeka ufaulu wa shule za Sekondari na kumaliza tatizo la vifo vya mama na mtoto katika Halmashauri hiyo kwa muda wa miezi saba.

"Haijawahi kutokea halmashauri hii kutokuwepo watoto wenye zero, lakini Sasa hivi wanafunzi wamefaulu daraja la kwanza na la pili shule zote za Sekondari, huyu Mkurugenzi ameleta Mapinduzi makubwa sana lazima aache alama kwenye wilaya yetu, maana ni mfano wa kuigwa".

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Renetus Mchau amewataka watumishi kuwa waadilifu ili waweze kutoa huduma kwa weredi na kuzingatia kanuni za utumishi hali itakayochochea matokeo chanya.


Tuesday, August 6, 2024

TIRA WAJA NA MIKAKATI UHAMASISAJI BIMA YA AFYA, KILIMO

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imekuja na mikakati ya uhamasishaji wakuu wa mikoa na wilaya kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na umuhimu wa kukata bima za afya majanga ya moto na sekta ya kilimo katika uzalishaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Agosti 6, 2024 Kamishna wa Bima nchini, Baghayo Saqware amesema lengo la kukutana na wakuu wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuhamasisha kuhusiana na utekelezaji wa sheria ya bima ya afya kwa wote.

Mbali na hilo pia kutambulisha ofisi za Kanda na majukumu ya Mamlaka hiyo kwa ili waweze kuwa mabalozi kwa wananchi wanao wasimamia kutumia bidhaa za bima.

DKT. TULIA WANANCHI TOENI TAARIFA ZA WAOMBA RUSHWA WASHUGHULIKIWE

Mbunge wa Mbeya mjini na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amewataka wananchi jijini hapa kutoa taarifa za siri za viongozi wanaoshawishi kutoa Rushwa wakati wakihitaji huduma.

Dkt. Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ametoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ofisi za CCM kata ya Kalobe Jijini hapa.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya mmoja wa wakazi wa kata hilo kueleza kuwepo kwa baadhi ya viongozi kutaka rushwa pindi wanapokwenda kuhitaji huduma.

RAS KILIMANJARO AWATAKA WAANDISHI KUCHAGIZA MAENDELEO

 Serikali mkoani Kilimanjaro imewataka waandishi wa habari mkoani humo kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali katika kuchagiza  maendeleo ya mkoa huo kwa kuwa vyombo vya habari vinayo nafasi kubwa ya kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana mkoani humo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro (RAS) Kiseo Yusuph Nzowa amesema hayo wakati akimkaribisha Balozi wa Sweden Mh. Charlotta Ozaki alipotembelea Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kilimanjaro (MECKI).

Nzowa amewapongeza waandishi wa habari mkoani humo kwa kuandika habari chanya zinazochochea maendeleo ya mkoa huo.

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA (TIRA) YAANZA ZIARA MKOA WA SONGWE


Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania(TIRA) imeanza ziara kuwatembelea Wakuu wote wa Mikoa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa lengo kuitambulisha Mamlaka na utekelezaji wa majukumu mbalimbali yanayotekelezwa nchini.

Ziara hiyo inaongozwa na Kamishina wa Bima nchini Dkt Baghayo Saqware akiambatana na wataalam katika vitengo mbalimbali na Viongozi wa Kanda.

Akiwa Mkoa Songwe mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo, Dkt. Baghayo Saqware amesema lengo la Mamlaka ni kuwahamasisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Bima ya afya kwa wote pili kutambulisha ofisi za Mamlaka za Kanda pamoja na majukumu ya Mamlaka kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya tatu kutoa elimu ya bima kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ili waweze kuwa mabalozi kwa wananchi wanaowasimamia kwa kuwahamasisha kutumia bidhaa na huduma za bima.

BALAOZI WA SWEDEN NCHINI TANZANIA ATEMBELEA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI KILIMANJARO

Agosti 05, 2024 Balozi wa Sweeden nchini Tanzania Mh. Charlotta Ozaki Macias ametembelea Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na klabu hiyo pamoja na kufanya mazungumzo na wanachama wa mkoa huo.

Mh. Balozi huyo pia ametaka kujua mchango wa MECKI kwa jamii katika kupaza sauti ili kuibua changamoto zilizopo kwenye jamii na namna klabu hiyo ilivyojipanga kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa 2025.

Pamoja na mambo mengine Balozi na wanachama hao wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na namna ya kuandika habari za uchaguzi.

Pia Charlotta ameambatana na timu kutoka Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) iliyokuwa ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Kenneth Simbaya.


Monday, August 5, 2024

DKT. TULIA AFANIKISHA MATIBABU YA MTOTO MWENYE UVIMBE SHINGONI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson,  amefanikisha matibabu ya mtoto Debora Saimon (6) Mkazi wa Kata ya Iganzo Jijini Mbeya aliyekuwa akisumbuliwa na uvimbe shingoni.

Debora amepatiwa matibabu ya kuondoa uvimbe huo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ikiwa ni siku chache tangu afikishwe kwa Dkt. Tulia kwa ajili ya kupatiwa msaada wa matibabu.

Sunday, August 4, 2024

WAKULIMA WA NDIZI RUNGWE WATAKA VIWANDA KUONGEZA THAMANI MAZAO

Wakulima wa zao la ndizi na parachichi Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya wameeleza ukosefu wa viwanda vya kuongeza thamani mazao  imekuwa mwiba kwao kujikwamua kiuchumi.

Wamesema hali hiyo imekuwa ikipelekea kuzalisha kwa wingi mazao ya kimkakati kwa wingi huku changamoto ni ukosefu wa masoko ya uhakika hususani kwa zao la parachichi na kupelekea kuharibikia mashambani.

Mkulima Byaison Mbungula akizungumza na mwandishi wetu jana Jumapili Agosti 4, 2024  kwenye banda la  maonyesho ya sikukuuya wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale ambayo kikanda yanafanyika Mkoa wa Mbeya.

TaCRI YAJA NA MIKAKATI KUKABILIANA NA KONOKONO KWENYE KAHAWA


Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) imesema imekuja na mikakati ya kudhibiti wadudu waharibifu wa zao hilo wakiwepo konokono.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Kanda (TacRI) Dismas Pangalas kwenye viwanja vya John Mwakangale vya maonyesho sikukuu ya wakulima Nanenane ambayo  yanafanyika kikanda mkoani hapa.

Amesema wadudu aina ya konokono wamekuwa na athari kubwa na tathimini za awali zinaonyesha kuwepo kwa mashambulizi yanaweza kusababisha kupoteza miche ya kahawa huku asilimia mbili mpaka tatu uharibiwa.