Taasisi ya Tulia Trust imekabidhi mahitaji ya chakula kwa wahitaji Wilayani Rungwe kwaajili ya Sikukuu ya Krismasi.
Msaada huo uliokabidhiwa kwa kaya 13 ni pamoja na mchele, maharage na mafuta ya kula vyenye jumla ya thamani ya Sh. milioni 3.

Ofisa habari na Mawasiliano wa taasisi hiyo Joshua Mwakanolo amesema
walengwa walionufaika ni ambao walibainika kwenye siku saba za kukimbiza
bendera ya Upendo, Uwajibikaji na Mshikamano.
“Wahitaji hao walibainika kupitia mbio za bendera hiyo kutoka Tulia Trust zilizofanyika wilayani Rungwe zilizobeba Ujumbe wa kuhamasisha Upendo, Uwajibikaji na Mshikamano” amesema Mwakanolo.
Amesema mpango huo wa taasisi umetolewa kupitia program ya Tulia Trust Mtaani Kwetu ambayo inalenga kuwasaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Mwakanolo amesema mbali na misaada huo wa chakula pia wameanza ujenzi na
ukarabati wa makazi ya walemavu na wazee wanaoishi kwenye makazi
hatarishi.
“Kuna nyumba za mahitaji wiwili tumeanza ujenzi baada ya kubaini makazi yao sio salama na kuwa katika hatari na haya ni maelekezo ya Mkurugenzi wa taasisi Dkt. Tulia Ackson na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika kuisaidia jamii” amesema Mwakanolo.

Mwakanolo
amesema lengo la taasisi hiyo ni kuona jamii hususani wazee na walemavu
wanakuwa sehemu salama kama jamii nyingine ikiwa ni kuunga mkono
jitihada za Serikali kuondoa changamoto kwa watanzania wenye mahitaji.
Kwa upande wake kikongwe Never Kisuru (80) amemshukuru Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa moyo wa kujitolea kwa wenye mahitaji pasipo kujali itikadi vya vyama wala udini.
“Maisha yangu nilikuwa naishi kwenye nyumba ya mianzi lakini leo hii taasisi hii baada ya kunitembelea nimeanza kujengwa makazi bora ambayo yataniwezesha kuwa salama” amesema Kisuru.

No comments:
Post a Comment