Wednesday, December 20, 2023

MTANILA AMCOS CHUNYA KULIMA HEKTA 1,428 ZA TUMBAKU MSIMU WA 2024/2025.

Wakulima wa zao la Tumbaku Kata ya Lupa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya wanatarajia kulima hekta 1428 sawa na ekari 3,571 za zao hilo kwa msimu wa kilimo 2024/25.

Hatua hiyo itapelekea kuchuma kilo milioni 1.3 mpka milioni mbili za tumbaku ambazo zitauzwa kwenye masoko ya uhakika ya ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku (Mtanila AMCOS) Isaya Hussein amesema kwenye Mkutano mkuu wa mwaka uliolenga kupitia taarifa za utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo katika umoja huo.

“Katika ekta 3,571 zitakazolishwa tunatarajia kupata kilo milioni 1.5 mpaka milioni mbili kwa msimu wa kilimo 2024/25 sambamba na kupanda miti 714,000 huku miti 116,000 imezalishwa kwenye shamba la chama cha ushirika huo” amesema.

Hussein amesema ili kufikia malengo waliyokusudiwa wameweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo za kilimo ambapo mpaka sasa wamepokea  mbolea aina ya NPK mifumo 15,070 na UREA 3,571 huku changamoto ikiwa kwenye mbolea ya CAN.

“Mbali na changamoto zikizopo kama ushirika tumeweka mikakati ya kusimamia usambazaji na kutoa maelekezo ya namna bora ya matumizi ya pembejeo za kilimo kwa wakulima wetu” amesema.

Amesema mikakati mingine ni kutoa elimu kwa wakulima kutambua umuhimu wa kujiwekea akiba, sambamba na wataalam wa kilimo kuwafikia kwa ajili ya kutoa elimu ya kilimo bora chanye tija kubwa.

Hussein amesema pia wameweka malengo kwa mwaka 2025/2026 kuongeza uzalishaji wa zao la tumbaku kutoka kilo milioni mbili  mpaka milioni tatu sambamba na upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya pembejeo za kilimo.  

Wakati huo huo amesema kufuatia taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuwepo kwa mvua nyingi wameweka utaratibu wa mfuko wa maafa ambao utasaidia wakulima watakao kubwa na athari za mvua ili kupunguza hasara na kufanya maandalizi msimu ujao.

“Tutakuwa na mwongozo kwa wakulima kuchanga fedha kwa ajili ya kusaidia wenzetu wataokubwa na majanga ya mvua, ili kuwasaidia kufanya maandalizi katika msimu ujao ili kuepuka madhara yaliyojitokeza msimu wa mwaka jana kwa wakulima kukata hasara kufuatia mvua kubwa ya mawe kunyesha na kuharibu majani ya tumbaku huku wakulima kukosa bima ya mazao” amesema.

Naye Mkulima na Mwanachama wa AMCOS hiyo, Matha Mwasenga ameomba Serikali kuharakisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati kwani kuna changamoto ya ucheleweshwaji hususan mbolea ya UREA

“Mbolea ya UREA ina umuhimu mkubwa sana kwenye kilimo cha zao la Tumbaku kwa msimu huu upatikanaji wake umekuwa wa shinda licha ya AMCOS yetu kuanzisha mfuko binasfi ambao umekuwa mkombozi kwetu” amesema.  

Kwa upande wake Mwakilishi wa Meneja Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Chunya (CHUTCU) Juma Shishi amesema ni kweli changamoto ya mbolea ilikuwepo huku akifafanua limeshafanyiwa kazi huku asilimia 95 zimeanza kufikishwa kwa wakulima ikiwepo mbolea ya CAN ambaye mahitaji yake ni makubwa.

No comments:

Post a Comment