Thursday, December 14, 2023

TULIA TRUST YAHITIMISHA ZOEZI LA KUPEPERUSHA BENDERA YA UPENDO.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo (kulia) akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wodi ya mama na mtoto katika Hosptali ya Makandana Wilaya ya Rungwe Mkoa Mbeya jana Alhamisi Desemba 13, 2023.

Taasisi ya Tulia Trust jana imehitimisha zoezi la kupeperusha bendera yenye ujumbe maalum wa Upendo, Uwajibikaji kwa jamii Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya ambayo ilianza kupeperushwa Desemba 9 mwaka huu.

Ofisa Habari na Mawasiliano, Joshua Mwakanolo amesema leo wilayani humo wakati akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya  Wilaya ya Makandana.


Mbali na kukabidhi mahitaji hayo pia wameshiriki kufanya usafi na kutoa misaada mbalimbali kwa jamii wakiwepo watu wenye ulemavu, wazee vikiwepo viti mwendo vyenye lengo la kuhitimisha ujumbe wa kuikumbusha jamii masuala ya upendo na uwajibikaji.

“Tumepeperusha bendera kwa muda wa siku saba ikiwa ni kutekeleza maagizo ya Mkurugenzi wetu, ambae pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, Dkt. Tulia Ackson” amesema.

Mwakanolo amesema mbali na kutoa misaada hiyo na kushiriki shughuli za kijamii, bado tumeendelea kupokea simu mbalimbali za wahitaji ambao tutawafikia baada ya kuwasilisha ombi hilo kwa Mkurugenzi wetu.

Mganga mfawidhi wa Hosptali ya Wilaya ya  Makandana, Dkt. Enock Mbikilwa ameishukuru Taasisi hiyo kwa kutoa mahitaji, na kwamba bado kuna changamoto mbalimbali ikiwepo uchakavu wa miundombinu.


 

No comments:

Post a Comment