Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu amezindua zoezi la ugawaji wa Vitambulisho Taifa (NIDA) leo Desemba 5, 2023.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Kata ya Kyimo wilayani humo, Haniu ameeleza kuwa jumla ya vitambulisho 69638 vitatolewa kwa Wakazi wa wilaya ya Rungwe huku Kata ya Kyimo ikipokea jumla ya vitambulisho 2850.

Haniu ameeleza kuwa uwepo wa kitambulisho kwa kila mkazi utasaidia kupata huduma mbalimbali kama za kibenki, mawasiliano na vitambulisho vya bima ya afya na hivyo kila mmoja hana budi kuvitunza kwani serikali imetumia gharama kubwa kuvitengeneza.
Pia Haniu amekemea vitendo vya kukaribisha wageni kutoka katika mataifa ya jirani bila kufuata utaratibu na kuwa kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa wananchi na mali zao, huku akiwaagiza watendaji wote wanaofanikisha upatikanaji wa vitambulisho kutoandikisha watu kutoka mataifa ya jirani.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mpokigwa Mwankuga amepongeza Serikali kwa kazi hiyo nzuri hatua itakayosaidia upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi hasa katika msimu huu wa kilimo.
No comments:
Post a Comment