Friday, December 1, 2023

DC RUNGWE AKEMEA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO.

Jaffary Haniu, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jaffary Haniu amekemea vitendo vya ukatili kwa watoto na jamii kwa ujumla ambavyo kwa namna moja au nyingine vinachangia kuongezeka kwa maambukizi ya UKIMWI.

Akihutubia katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo kwa Mkoa ya Mbeya yamefanyika Wilayani Rungwe, Haniu ametaja vitendo ukatili kuwa ni pamoja na ubakaji ulawiti na ukeketaji katika baadhi ya  mikoa nchini Tanzania.

Haniu amehamasisha wananchi kujitokeza kupima afya zao mara kwa mara ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya maendeleo.
Ameongeza kuwa serikali imekuwa ikitoa elimu kwa jamii kuanzia ngazi ya kaya pamoja na kutoa dawa kwa ajili ya kufubaza virusi vya UKIMWI.

Mganga Mkuu mkoa wa Mbeya Dkt. Maisara Karume ametaja juhudi zinazofanywa na Mkoa katika kutokomeza ugonjwa huo 8ni pamoja na kufanya tohara kwa wanaume ambayo imethibika kuwa ina uwezo wa kuzuia maambukizi kwa asilimia 60%, pia kutoa elimu na matumizi ya kondomu na kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua.

No comments:

Post a Comment