Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani ambae pia ni Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amelazimika kuingilia kati mgogoro wa Kanisa la The Children of Gospel for All International (TCH-GOLFN) na Halmashauri ya Jiji la Mbeya unaohusisha uhalali wa umiliki wa eneo linalopaswa kujengwa kanisa na kuweka zuio kwa kipindi kirefu sasa.
Dkt. Tulia ambae pia ni Mbunge wa Mbeya mjini amefikia hatua hiyo baada
ya kusikia uwepo wa mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya 20 ukihusisha
Halmashauri ya Jiji na kusababisha waumini wa kanisa hilo kutaka kumuona
Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati.
Akizungumza na waumini
wa na Mchungaji wa kanisa hilo, John Ikowelo katika eneo lenye mgogoro
Dkt. Tulia ametaka uongozi wa Jiji la Mbeya kupelekea nyaraka mbalimbali
zinazoonyesha uhalali wa nani mmiliki wa eneo hilo.
Awali
Mchungaji Ikowelo alimuonyesha Dkt. Tulia nyaraka mbalimbali za eneo
hilo zikiwepo ambazo zilimtaka mchungaji huo kulipia gharama za kibali,
hususani majina ya wananchi walio eneo kwa ajili ya kanisa na vikao
mbalimbali vilivyobariki kuwepo kwa ujenzi wa nyumba hiyo ya ibada.
“Mh
Spika na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwanza unisamehe
nilikuruka kutoa taarifa za mgogoro huu kwako, pia waumini na uongozi wa
kanisa tumekasirika sana na Serikali sababu kubwa ni watendaji wenu wa
ngazi za chini ni shida sana na kuwa chanzo cha mgogoro” amesema
Mchungaji Ikowelo.
Amesema kwa kuzingatia nyaraka hizo anaomba
busara ya Serikali kuingilia kati ili haki itendeke wapewe kibali
sambamba na kueleza kuna ujanja unaotaka kufanywa dhidi ya haki ya
kanisa.
Kufuatia kauli hiyo, Dkt. Tulia alilazimika kumbana Ofisa
mipango miji, Esau Dickley aeleze sababu za kutokutoa kibali cha ujenzi
wa kanisa hilo, huku kukiwa na nyaraka mbalimbali za kubariki mradi wa
nyumba ya ibada na viongozi mbalimbali wa serikali waliopita wakiwepo wa
ngazi za serikali za mitaa.
“Sasa Leo nilikuja kwa ajili ya
kutembelea kujiridhisha na kutoa maelekezo lakini sitoweza kwa sababu
kuna mkanganyiko, mchungaji anazo nyaraka zote zinazo onyesha eneo hilo
liko kisheria, sasa niwatake Jiji rejeeni na vielelezo vyote ili niweze
kufanya maamuzi na haki itendeke.” amesema.
Dkt. Tulia amesema
mara baada ya taarifa za Jiji kuwa tayari utaitishwa mkutano wa hadhara
wa wananchi na kumtaka mchungaji kuja na watu waliotoa eneo kwa ajili ya
ujenzi wa kanisa sambamba na wenyeji wanaojua historia ya eneo hilo.
Naye
Naibu Meya wa Jiji la Mbeya, Kefasi Mwasote amehaidi kutoa ushirikiano
wa kuhakikisha mgogoro huo inafikia kikomo sambamba na kuzisaka nyaraka
zote tangu mgogoro huu kuanze miaka 20 iliyopita.
Naye Ofisa
Mipango miji Jiji la Mbeya, Dickley amesema mgogoro huo ameugundua tangu
mwaka 2017 ambapo lilipimwa na kubainika kuwa ni la shule.
Amesema
kuwa Mchungaji alienda kuomba kibali ambapo wameshindwa kutokana na
kubaini eneo hilo ni eneo Oevu sambamba na Jiji kuja na mipango kabambe
wa mwaka 2025/30.
“Ili eneo lilipimwa na kupendekezwa
litaendelezwa mpango kabambe la eneo oevu tangu mwaka 2019” Jambo ambalo
lilipeleke Spika Dkt. Tulia kuhoji mpango huo ulipitishwa na nani awali
ambalo limekosa majibu ya kujitoshereza na kutengeza mashaka.
No comments:
Post a Comment