Saturday, December 9, 2023

VICOBA KUWAKOMBOA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA.

 
Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo amepongeza kitendo cha baadhi klabu za waandishi wa habari nchini kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa (VICOBA).

Akiongea mara baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho ya klabu hizo yaliyofanyika Desemba 09, 2023 katika viunga vya ofisi ya UTPC Nsokolo amesema kuanzishwa kwa VICOBA kutasaidia waandishi kuendelea kutimiza wajibu wao  wa kuitumikia jamii mbali na kucheleweshwa kwa kupata stahiki zao."Waandishi wa habari wamekopa kwenye VICOBA na kutumia zile fedha kwenye kilimo, biashara na shughuli nyingine ambazo zinawaingizia kipato na kuwaendeleza wao na familia zao, lakini pia fedha hizo zinawawezesha kufuata habari katika maeneo ambayo yanahitaji nauli na gharama nyingine".

Pia amepongeza baadhi ya klabu zilizoshiriki katika kampeni mbalimbali za kuifanya jamii kuwa na afya nzuri kwa kuandika habari zinazohusu masuala ya afya, elimu, uchumbi na mengineyo.

Nae Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya amepongeza ubunifu uliofanywa na klabu katika maonyesho hayo kwani imeonyesha namba klabu zinavyoweza kubadilika na kuanza kujitegemea.

Simbaya amewapongeza SIDA ambao ndio wafadhili wa UTPC kwa kuwezesha kutekelezwa kwa shughuli mbalimbali kwa muda mrefu.

“Hivyo tunawapongeza wafadhili wetu ambao ni SIDA na mwakani tutakuwa na maonyesho kwa kuwashirikisha watu wa kutoka nje na tasnia ya habari ili waje wajionee namna ya ushirikiano wetu” amesema Simbaya.

Baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo wamesema klabu zimekua zikipaza sauti za wananchi na kuziandika kwenye vyombo vya habari mbalimbali ambapo serikali na wadau huzitafutia ufumbuzi.

Mwekahazina wa klabu ya waandishi wa habari kutoka visiwani Zanzibar Rahima Suleiman amesema katika maonyesho hayo amejifunza namna klabu nyingine zinavyofanya kazi za mradi mbalimbali ambapo wengine wameanzisha vikundi vya VICOBA, bajaj na bodaboda.

No comments:

Post a Comment