Wakaguzi wa Kata nane Mkoani Mbeya wamekabidhiwa pikipiki aina ya Boxer
kwa ajili ya kurahisisha na kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu
yao katika Kata hizo.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya pikipiki hizo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Benjamin
Kuzaga amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura
kwa kutambua umuhimu wa vitendea kazi katika kufanikisha utekelezaji wa
kazi mbalimbali kwa wakaguzi wa Kata.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Rungwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Philipo Mhako amemshukuru kupata pikipiki mbili ambazo zitakwenda kutatua changamoto ya usafiri kwa wakaguzi Kata kutoka na baadhi ya maeneo kutokufikika kwa urahisi.Mkaguzi Kata ya Madibila iliyopo Wilaya ya Mbarali, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Julius Mongo ameahidi kutumia pikipiki hiyo kuwafikia wananchi katika maeneo ya vijijini na kwenye vitongoji na kutoa elimu pamoja na kutatua kero mbalimbali za kiuhalifu na kijamii.
Jumla ya Wakaguzi nane wa Kata za Lufilyo na Masuku zilizopo Wilaya ya Rungwe, Kata ya Matema Wilaya ya Kyela, Kata ya Matwiga na Kambikatoto Wilaya ya Chunya, Kata ya Ikukwa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi na Kata ya Madibila Wilaya ya Mbarali wamekabidhiwa pikipiki awamu hii ya kwanza.
No comments:
Post a Comment