Taasisi ya Maryprisca Women Impowerment Foundation (MWEF) inayoongozwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi imetembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa ajili ya kutoa msaada kwa wazazi waliojifungua siku ya sikukuu ya Christmas.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Maryprisca Women Impowerment Foundation Adam Simbaya amesema lengo la kutembea Hospitali ya wazazi Meta ni kumshukuru Mungu pia akianisha zawadi zilizotolewa kuwa ni pamoja na maziwa, sabuni, pampas na wipes.
Aidha Simbaya amesema wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye amekuwa akiyagusa makundi mbalimbali yakiwemo ya wanawake na watoto.
Friday, December 27, 2024
MWEF YATOA MSAADA KWA HOSPITALI YA WAZAZI META
Sunday, December 15, 2024
JAJI MWAMBEGELE "KUJIANDIKISHA KUWA MPIGA KURA ZAIDI YA MARA MOJA NI KOSA LA JINAI"
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Jacob Mwambegele katika Mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura umefanyika Jijini Mbeya leo Disemba 15, 2024.
"Kujiandikisha kuwa mpiga kura zaidi ya mara moja ni kosa la jinai, 'mtu yeyote atakaeomba kuandikishwa zaidi ya mara moja atakuwa ametenda kosa la jinai na akitiwa hatiani adhabu yake ni faini isiyopungua kiasi cha shilingi laki moja na isiyozidi laki tatu au kutumikia kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miaka miwili gerezani au vyote kwa pamoja" amesema Jaji Mwambegele.
Thursday, December 12, 2024
DKT. TULIA APOKEA MASHINE YA UPASUAJI NA KITANDA KWA WAJAWAZITO
Vifaa hivyo vimetolewa kwa kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya vilovyotolewa na wadau wa Maendeleo.
Dkt. Tulia amepokea vifaa hivyo kutoka kwa mwakilishi wa wadau hao Noelah Msuya jana Desemba 12, 2024 na kisha kukabidhi kwa uongozi wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa.
Dkt,Tulia ameipongeza Serikali kwa jitihada zake endelevu katika kuboresha sekta ya afya ikiwemo kujenga vituo vya afya ili kuwasogezea wananchi wake huduma ya karibu.
WAKULIMA WATAKIWA KULIPA MADENI MSIMU 2023/24
Chama cha Msingi cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku (Lualaje Amcos) kimewataka wakulima kulipa madeni kwa wakati ili kuepuka kupigwa mnada kwa mali zao ikiwepo mashamba .
Mwenyekiti wa Lualaje Amcos, Alberto Kacheza amesema leo Desemba 12, 2024 kwenye mkutano mkuu 41 wa mwaka wa kupitia taarifa mapato na matumizi hali ya uzalishaji kwa msimu huu wa kilimo.
Kacheza amesema kuna baadhi ya wakulima kwa makusudi wamekuwa wakilimbikiza madeni ya mikopo ya pembeo kwa makusudi hali inayopelekea kupata hati za mashaka
"Leo tumepitia taarifa mbalimbali sambamba na mwenendo Amcos yetu na kupendeleza masuala ya msimu wa kilimo 2024/25 katika uwekezaji wenye tija kwenye kilimo cha tumbaku na hatua za kuwachukulia wakulima wasiorejesha fedha za mikopo" amesema.
Friday, December 6, 2024
MHANDISI MARYPRISCA MAHUNDI ACHANGIA MIL. 3.4 NA TOFALI KIKUNDI CHA GWALUGANO ISANGE
Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameunga mkono juhudi za Kikundi cha UWT Gwalugano Isange chenye mtaji wa shilingi milioni tisini huku akikichangia shilingi milioni tatu na laki nne pia tofali elfu moja za saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mradi.
Katika hotuba yake Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wanawake kupendana na kuwataka waendelee kuwahamasisha wengine kujiunga ili kila mwanamke amiliki uchumi wake ambapo amewataka wanawake kuchangamkia mikopo inayotolewa na Halmashauri.
Mbali ya kukipongeza kikundi hicho amesema changamoto wazichukulie kama fursa akikazia kampeni yake ya wanawake na uchumi pia akiwahimiza kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan.
Friday, November 29, 2024
WENYEVITI WAONYWA KUTOKUWA CHANZO CHA MIGOGORO
Monday, November 25, 2024
BENKI YA PBZ YAUNGA MKONO UMOJA WA BAJAJI NA BODABODA
Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) imetoa pikipiki 10 zikiwepo za matairi matatu (bajaji) mbili kwa umoja wa bajaji na bodaboda jiji la Mbeya kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali kuwezesha vijana kujiajiri
Meneja Masoko na Uendelezaji wa Benki ya PBZ Mohamed Ismail amesema jana Novemba 25, 2024 mara baada ya kumkabidhi Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackon kwenye maadhimisho ya miaka 15 ya umoja wa bajaji Jiji la Mbeya yaliyo fanyika viwanja vya Mwenge.
Ismail amesema kwa kutambua vijana ni chachu ya maendeleo na namna gani Mbunge wetu na Spika Dkt. Tulia Ackson anavyowekeza kusaidia vijana kujiajiri.
DKT. TULIA, TFS WAZINDUA KAMPENI UPANDAJI MITI MILIONI MBILI
Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Dkt. Tulia Ackson amehamasisha jamii kugeukia matumizi ya nishati safi na kutunza mazingira kwa kupanda miti rafiki.
Dkt. Tulia ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) amesema jana Jumatatu Novemba 25, 2024 wakati uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji upandaji miti iliyohusisha Wakala wa Huduma za Misitu (TFS).
Amesema katika kampeni hiyo wanatarajia kupanda miti milioni mbili ya kivuli yenye uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Kampeni hiyo imehusisha upandaji miti katika Taasisi za Serikali zikiwepo Shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Mbeya na kugusa kata 36.
JESHI LA POLISI MBEYA LATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI
Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 nchini, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendesha mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari mkoani humo kuhusu masuala ya uchaguzi.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Novemba 23, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania Tawi la Mbeya, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amesema kuwa Jeshi la Polisi lipo imara kuhakikisha linasimamia sheria, kanuni na taratibu wakati wa uchaguzi na halitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kukiuka.
Kamanda Kuzaga amewataka Waandishi wa Habari kuwa wazalendo na kutumia taaluma yao kuwajulisha wananchi mchakato mzima wa uchaguzi jinsi unavyoenda na kutoa elimu kuhusu haki na wajibu wa mpiga kura.
DKT. TULIA ACKSON ASHIRIKI IBADA MADHABAHU YA SAUTI YA UPONYAJI NA REHEMA ISYESYE JIJINI MBEYA
Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson ameshiriki ibada Kanisa la Baptist Isyesye Madhabahu ya Sauti ya Rehema na sauti ya uponyajiKata ya Isyesye huduma inayoongozwa na Mchungaji Patrick Mwalusamba ambapo amewahimiza Waumini kuendelea kuombea amani nchini huku akiwasisitiza kushiki uchaguzi utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Dkt. Tulia Ackson amesema Waumini wanawajibu wa kwenda kusikiliza kampeni za uchaguzi ili wapate viongozi watakaowaletea maendeleo katika mitaa yao. Pia ameipongeza huduma hiyo kwa namna inavyozidi kukua siku hadi siku.
Dkt. Tulia Ackson amesema Waumini wasiposhiriki kupiga kura wasiwe na sababu za kuwalaumu viongozi watakaochaguliwa kwa kuwa wao wameshindwa kuitumia fursa hiyo.
UTPC KUZINDUA KAMPENI YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA NOVEMBA 25, MKOANI MANYARA
Kuelekea Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umejipanga kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kupitia mtandao wa WhatsApp, pamoja na mitandao mwingine ya kijamii kwa kushirikiana na klabu 28 zilizopo mikoa yote ya Tanzania . Kampeni hii itazinduliwa rasmi Novemba 25 Mkoani Manyara.
Friday, November 22, 2024
CHAUMA KUFANYA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KIDIGITALI
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Mkoa wa Mbeya Ipyana Njiku amesema chama hiyo kimeamua kufanya kampeni kidigitali kwa kupita mitaani na kipaza sauti ili kutokuleta usumbufu kwa wananchi wakati wakiendelea na shughuli zao.
WAPINZANI WASHINDWA KUSIMAMISHA WAGOMBEA KWENYE MITAA 53 MBARALI
Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mkoa wa Mbeya Bahati Ndingo amesema wamejipanga CCM kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024 na kuwataka wananchi kuendelea kukiamini.
Ndingo amesema jana Novemba 21, 2024 wakati wa uzinduzi wa kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo zilizo fanyika katika kata ya Ubaruku huku mgeni rasmi akiwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa.
"Tuna uhakika Mbarali kushinda kwa kura za kishindo uchaguzi wa serikali za mitaa wagomea tulio wasimamisha tuna imani nao kwa asilimia 100 na kwamba mitaa 53 watapita bila kupingwa baada ya upinzani kutosimamisha wagombea" amesema Ndingo.
Wednesday, November 20, 2024
MSD MAKAO MAKUU WATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA KUJIONE HUDUMA ZINAZOTOLEWA
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo Novemba 20, 2024 imetembelewa Ujumbe maalumu kutoka Bohari ya Dawa (MSD) ulioambatana na mjumbe wa bodi, uongozi wa juu wa bohari ya Dawa kutoka makao makuu pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Kanda ya Nyanda za juu kusini.
Lengo la ujumbe huo kutembelea hospitalini hapa ni kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa kupitia ushirikiano uliopo pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali kwa lengo la kuboresha maeneo mbalimbali ya utoaji huduma kupitia mapungufu yanayojitokeza ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kuwekaza jitihada mbalimbali katika ubunifu kupitia wataalamu wa ndani ili kupunguza gharama mbalimbali zinazoweza kujitokeza hasa katika swala la uboreshaji na ukarabati wa vifaa tiba pindi vinapopata hitirafu.
Thursday, November 14, 2024
WAMUOMBA MBUNGE KUKAMILIKA JENGO KITUO SHIKIZI
Wananchi wa kijiji cha Mpolo Wilaya Mbarali Mkoa wa Mbeya wameomba Mbunge wa Jimbo hilo, Bahati Ndingo kuwasaidia kukamilisha jengo la kituo cha elimu shikizi ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi.
Ombi hill wamelitoa jana Novemba 14, 2024 kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge huyo uliolenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Mkazi wa kijiji cha Mpola Shija Masanja amesema ukosefu wa shule shikizi umepelekea watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu.
Wakati huo huo wameomba kuboreshwa miundombinu ya barabara, umeme kijijini hapo ili kuwasaidia kuchochea shughuli za kiuchumi.
TDB KUHAMASISHA PROGRAMU YA UNYWAJI WA MAZIWA KUKABILIANA NA UDUMAVU
Serikali kwa kushirikiana na Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) imekuja na programu ya uhamasishaji unywaji maziwa ikilenga kuwafikia wanafunzi 100,000 katika shule 140 nchini.
Programu hiyo imefika katika mikoa nane ukiwepo Mkoa wa Mbeya sambamba na kutengeneza fursa ya usambazaji kwa wasindikaji wadogo kufikisha huduma mashuleni.
Kaimu Meneja wa Bodi ya Maziwa, Joseph Semu amesema jana Novemba 14, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wa programu hiyo kwa Mkoa wa Mbeya.
Monday, November 11, 2024
DKT. TULIA AWASHUKIA WANAO TELEKEZA WAZAZI KWA IMANI POTOFU
Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson amekemea tabia ya baadhi ya familia kuwa na utamaduni wa kutelekeza wazazi kwa kutanguliza imani za kishirikina.
Dkt. Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mbunge Duniani (IPU) amesema jana Novemba 11, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa mtaa wa Inyara Kata ya Iyunga.
Kauli ameitoa wakati akikabidhi nyumba kwa wajane Tusekile Lumbalile (88) na Mwaine Lumbalile (86) ambao ni ndugu wa familia moja wanaoishi bila msaada wa familia.
"Ndugu zangu inaumiza sana hawa wakina mama walipaswa watunzwe na familia zao lakini wanaishi peke yao huku changamoto ni kujengeka na kuamini imani potofu za kishirikina" amesema.
Tuesday, November 5, 2024
CHINA YAINGIA MAKUBALIANO NA TAASISI YA TULIA TRUST KUKUZA UTAMADUNI
Taasisi ya Tulia Trust imeingia makubaliano na kikundi cha ngoma za asili cha Wu Opera kupitia kituo cha Zhejiang Wu Opera Research Centre Of China kwa lengo la kukuza utamaduni baina ya nchi hizo mbili.
Taasisi hiyo ambayo Mkurugenzi wake Spika wa Bunge Mbunge wa Mbeya mjini na Rais wa Umoja wa Mabunge Dunuani (IPU) Dkt. Tulia Ackson imeingia makubaliano hayo leo Novemba 4, 2024.
Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo amesema lengo ni kukuza utamaduni na asili baina ya nchi ya Tanzania na China kubadilishana tamaduni zetu, lugha na mtindo.
Tuesday, October 29, 2024
WASHINDI TULIA STREET TALENT COMPETITION 2024 KUPELEKWA BAGAMOYO
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge na Mbunge Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson amesema walioibuka washindi mashindano ya Tulia Street Talent Competition kuendelezwa kituo cha sanaa na utamaduni Bagamoyo.
Dkt. Tulia amesema Oktoba 27 mwaka huu wakati wa kuhitimisha mashindano hayo huku mgeni rasmi msanii mkongwe Naseeb Abdul (Diamond Platnam) ambayo yalifanyika kwa siku tatu mfurulizo ikiwa ni msimu wa tano.
"Sisi kama Tulia Trust tunawa andaa na kuibua vipaji ili watakao wahitaji watawatafuta lakini pia niombe Daimond useme neno ili vijana hawa wapone" amesema.
CUoM WAADHIMISHA MIAKA 25 KUMBUKIZI LA MWALIMU NYERERE
Chuo Kikuu Katoriki Mbeya (CUoM) kimefanya kongamano la kumbukizi la miaka 25 ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama sehemu ya kuenzi mchango wake katika kulitumikia taifa.
Kongamano hilo limefanyika Oktoba 25 mwaka huu huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere lililoshirilisha wadau wakiwepo wanafunzi maprofesa na madaktari kutoka vyuo mbalimbali.
Akizungumza kwenye kongamano hilo Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Rumuald Haule amesema uongozi wa chuo unatambua mchango mkubwa wa hayati Mwalimu Nyerere katika kusimamia sekta ya elimu ya ujamaa na kujitegemea.
Thursday, October 24, 2024
SERIKALI KUTUMIA BILIONI 133.3 KWAAJILI YA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WAJASILIAMALI WADOGO NA WA KATI
CHAUMA YAWAITA VIJANA NA WANAWAKE KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI
Njiku ametoa rai hiyo wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu maandalizi ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa
Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji utakaofanyika Novemba 27, 2024.
"Tumeona muamko mdogo wa watu kujitokeza kupiga kura lakini niwambie hii ni haki yetu ili kupata viongozi bora kwa maendeleo ya taifa letu", amesema Ipyana Njiku.
Pia Njiku amewataka wananchi kuwa chachu ya kutunza amani
ya nchi wakati na baada ya chaguzi ili kuendelea kuwa Taifa moja na
kuwaalika wenye nia na uwezo kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama hicho.
"Haki ya kupiga kura ni silaha muhimu kwa kila raia katika kuhakikisha uongozi bora maendeleo yetu, bila kura unatoa nafasi kwa wengine kuamua nani awe kiongozi wao kwahiyo tunaomba siku ya uchaguzi tujitokeze kwa wingi kwenda kuchagua viongozi bora. Pamoja na kupiga kura lakini hii ni fursa kwa watu wenye sifa, dhamira safi, uadilifu na utayari kuwatumikia wananchi kwa kujitokeza kugombea kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMMA", amesema Njiku.
DKT. TULIA AGAWA MITUNGI YA GESI KWA MAMANTILIE WA SOKO LA MATOLA
Mbunge wa Mbeya mjini na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amegawa mitungi ya nishati gesi bure kwa mamantilie 25 katika soko la Matola jijini hapa.
Hatua ya Dkt. ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Dunia (IPU) kugawa mitungi na nishati safi ya gesi ni kuhamasisha mama lishe kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo sio salama kwa afya.
Akizungumza mara baada ya zoezi la kugawa mitungi kwa Mama ntilie 25 amesema hiyo ni sehemu ya ahadi yake lakini pia ni kuunga mkono juhudi za Mh Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo.
Wednesday, October 23, 2024
MADIWANI CHUNYA WAMNG'OA MTENDAJI KIJIJI KWA UTORO
Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya limemwazimia kumfukuza kazi Ofisa mtendaji wa kijiji cha Matwiga Samweli Koko kwa madai ya kukithiri kwa vitendo vya ulevi, utoro na matumizi mabaya ya madaraka.
Hatua hiyo imefikiwa jana Oktoba 22, mwaka huu baada ya kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu kukutana kujadili bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 sambamba na kufanya maamuzi kuhusiana na tuhuma hizo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chunya, Ramadhan Shumbi amesema wamefikia hatua hiyo kufuatia kukithiri kwa tabia hizo licha ya kumkanya mara kadhaa.
WANANCHI 188,644 WAJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA WILAYANI CHUNYA
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya Mubarak Batenga amesema asilimia 89 ya watu 188, 644 wameji andikisha kwenye daftari la wapiga kura na kutarajiwa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu.
Batenga amesema jana Oktoba 22, 2024 wakati akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya mwaka 2024/25 cha kujadili taarifa ya fedha na makusanyo ya mapato ya ndani huku wakiwa wamevuka malengo na kufikia Sh 12.5 bilioni.
Amesema kufuatia taarifa ya daftari la wapiga kula madiwani warejee kutoa elimu ya uhamasishaji ili wote waweze kupiga kura kuchagua wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa ifikapo Novemba 27 Mwaka huu.
Tuesday, October 22, 2024
MEYA ISSA: JIEPUSHENI KUREJEA MIAKA 10 ILIYOPITA
Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Dourmohamed Issa amewataka wananchi katika Jimbo la Mbeya mjini kutorejea miaka 10 iliyopita kwa kupiga kura kwa viongozi wasiofaa.
Issa amesema jana katika ziara ya Mbunge wa Mbeya Mjini Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwepo elimu na afya katika kata mbalimbali.
Amesema Taifa linaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na Mkuu 2025 hivyo wananchi wasifanye makosa badala yake wachague viongozi wa CCM akiwepo Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson na wenyeviti wa serikali za mitaa ambao wataleta tija katika maendeleo.
SPIKA KUCHANGIA SARUJI MIFUKO 200 SHULE YA TAMBUKA RELI

Rais wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson amechangia mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi matundu ya vyoo Shule ya Msingi Tambuka reli.
Dkt. Tulia ametoa ahadi ya mchango huo leo Oktoba 22, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya choo.
Amefikia katika hatua hiyo baada ya kubaini kuwa katika hali mbaya ya uchakavu wa miundombinu sambamba na matundu ya vyoo na majengo ambayo yana hararisha usalama wa wanafunzi.
Monday, October 21, 2024
BITEKO MGENI RASMI WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA MBEYA
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini Dotto Biteko anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa ambayo yatafanyika Mkoa wa Mbeya na kuhusisha Taasisi mbalimbali za kifedha.
Maadhimisho hayo yatafunguliwa rasmi kuanzia Oktoba 22 mpaka 26 mwaka huu katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20, 2024 Kamishna msaidizi wa Idara ya Uendeshaji sekta ya fedha kutoka wizarani Janeth Hiza amesema lengo ni kutekeleza mpango mkuu wa maendeleo ya sekta hiyo kwa mwaka 2020/21 na 2029/30.