Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson amekemea tabia ya baadhi ya familia kuwa na utamaduni wa kutelekeza wazazi kwa kutanguliza imani za kishirikina.
Dkt. Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mbunge Duniani (IPU) amesema jana Novemba 11, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa mtaa wa Inyara Kata ya Iyunga.
Kauli ameitoa wakati akikabidhi nyumba kwa wajane Tusekile Lumbalile (88) na Mwaine Lumbalile (86) ambao ni ndugu wa familia moja wanaoishi bila msaada wa familia.
"Ndugu zangu inaumiza sana hawa wakina mama walipaswa watunzwe na familia zao lakini wanaishi peke yao huku changamoto ni kujengeka na kuamini imani potofu za kishirikina" amesema.
Ameongeza "Namuomba Mungu hao watoto walio zaliwa na wazee, awatunze wapate familia ambazo wakifika nao uzeeni wawafanye kama wanavyo watenda wazazi wao" amesema.
Dkt. Tulia ameitaka jamii kuwa na utaratibu wa kisaidia wazee wasio jiweza na sio kuwaacha wakipitia maisha magumu kutokana na dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa wananchi na familia zao.
Mbunge wa Jimbo la Mbarali Bahati Ndingo amewataka wanambeya kuitumia tunu ya Dkt. Tulia kama mwanga katika kuisaidia jamii na kuleta maendeleo kwa wananchi.
"Mimi jimboni kwangu nahojiwa lini nitasaidia wananchi kama anavyofanya, Mbunge wenu niwasihi tu shikamane na kumuunga mkono" amesema Ndingo.

No comments:
Post a Comment