Monday, November 25, 2024

DKT. TULIA, TFS WAZINDUA KAMPENI UPANDAJI MITI MILIONI MBILI

Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Dkt. Tulia Ackson amehamasisha jamii kugeukia matumizi ya nishati safi na kutunza mazingira kwa kupanda miti rafiki.

Dkt. Tulia ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) amesema jana Jumatatu Novemba 25, 2024 wakati uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji upandaji miti iliyohusisha Wakala wa Huduma za Misitu (TFS).

Amesema katika kampeni hiyo wanatarajia kupanda miti  milioni mbili ya kivuli yenye uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Kampeni hiyo imehusisha upandaji miti katika Taasisi za Serikali zikiwepo Shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Mbeya na kugusa kata 36.

"Hii ni awamu ya pili awamu ya kwanza tulipewa miche ya matunda 8,000 na awamu hii  miti  ya vivuli milioni mbili, tuombe TFS msituchoke tutaomba tena" amesema Dkt. Tulia.

Hata hivyo Dkt. Tulia ameomba TFS kuona namna kutoa miti kwa ajili ya kupanda kwenye safu ya Mlima Kawetele ambako yalitolea maporomoko ya topee ikiwa ni kutekeleza ahadi ya serikali.

"Eneo la mlima Kawetere lina changamoto ya mazao kutostawi  tuombe TFS kufanya utafiti  kama wananchi wanaweza kupanda miti ya aina gani ambayo wataweza kuihudumia na kuvuna kwa kipindi cha miaka mitatu au mitano" amesema.

Kwa upande wake Kamishna wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema lengo ni kuunga mkono kampeni ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ili kulinda rasilimali za misitu.

Amesema kuwa amesema Spika Dkt. Tulia anafanya kazi kubwa kuhamasisha suala la utunzaji mazingira na misitu ya asili kwa lengo la kunusuru viumbe hai na upotevu wa rasilimali ya maji.

"Tulinde misitu ili kupata kivuli,matunda na uvunaji wa mbao na kujenga mazingira ya kuwezesha na kulinda viumbe  hai majini na rasilimali ya maji

Profesa Silayo amesema bila misitu kunakuwa na hewa chafu inayo sababisha magonjwa ndio sababu ya TFS kumeunga mkono kampeni ya serikali ya upandaji wa miti ili kulinda mazingira na kuhamasisha matumizi ya nishati safi .

"Mh Spika amesema lengo ni kupanda miti milioni mbili tunaunga mkono kwani amekuwa akipitisha sheria za uhifadhi wa mazingira katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi" amesema.

Chifu wa Mkoa wa Mbeya Rocket Mwansinga amesema wamepewa jukumu na serikali kutunza rasilimali za miti na kuonya waharibifu hususani wanaokata miti ovyo.

Mwashinga amesema yeye ni balozi wa misitu Mbeya mjini na kuwataka machifu kushirikiana kulinda misitu na kufichua watu wanaohujumu kwa kukata na kuharibu rasilimali hiyo.

"Tumepewa amri na serikali kutunza misitu ya asili ili kulinza na kunusuru upotevu wa rasilimali za maji kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS).

No comments:

Post a Comment