Thursday, December 12, 2024

DKT. TULIA APOKEA MASHINE YA UPASUAJI NA KITANDA KWA WAJAWAZITO

Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson, amekabidhiwa mashine ya upasuaji na kitanda cha kisasa kwa ajili ya wajawazito vyenye thamani ya Sh Milioni 102 .

Vifaa hivyo vimetolewa kwa kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya vilovyotolewa na wadau wa Maendeleo.

Dkt. Tulia amepokea vifaa hivyo kutoka kwa mwakilishi wa wadau hao Noelah Msuya jana Desemba 12, 2024 na kisha kukabidhi kwa uongozi wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa.

Dkt,Tulia ameipongeza Serikali kwa jitihada zake endelevu katika kuboresha sekta ya afya ikiwemo kujenga vituo vya  afya ili kuwasogezea wananchi wake huduma ya karibu.

"Pia niwashukuru wananchi na wadau kwa michango yenu kuwezesha upatikanaji wa mashine ya upasuaji ya kisasa na kitanda kama njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita" amesema Dkt. Tulia.

Mdau wa Maendeleo Noela Msuya amesema lengo kuchangia vifaa hivyo ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha huduma za wakimama wajawazito wakati wa kujifungua.

Amesema Mwaka 2020 katika Maadhimisho ya siku ya Mwanamke duniani Machi 8, 2020 walifanya harambee ya kuchangia huduma za afya na kupatikana kiasi cha Sh 110 milioni" amesema.

Msuya amesema ilipofika  mwaka 2023 waliweka fedha hizo kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja  (UTT -AMIS) ambapo walipata kiasi cha Sh 126 milioni sambamba na ongezeko la faida ya Sh 16 milioni.

Amesema kufutia hatua hizo waliwasiliana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kutimiza ndoto yao kuchangia huduma katika jengo la wakinamama na mifuko 448 ya saruji.

No comments:

Post a Comment