Katibu
Tawala Mkoa wa Mbeya Mohamed Fakii ameonya wenyeviti wa serikali za
mitaa kuepuka kuwa chanzo cha migogoro na badala yake kuimarisha ulinzi
shirikishi na usalama wa raia na mali zao.
Mohamed amesema leo Novemba 28, 2024 wakati akiwa mgeni rasmi kwa niaba
ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa kwenye tukio la kuapishwa
wenyeviti 181 na wajumbe 908 katika mitaa, vitongoji na kata.
Amesema wenyeviti baada ya kuapishwe wakawe chachu kwa wananchi na sio
kugeuka wababe wakati wa kuwatumikia makujumu yako kwenye maeneo yao ya
kazi.
"Mbeya tuna ushindi wa asilimia 95 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa
sasa baada ya kuapishwa rejeeni kutekeleza majukumu yenu kwa
kumtanguliza Mwenyezi Mungu" amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wake Mtaa wa Mwasyoge Limba Mwailubi
amesema wanakwenda kutekeleza majukumu yao kwa vitendo na kujipanga
katika uchaguzi Mkuu 2025.
"Tumeaminiwa na wananchi tumesikia maelekezo ya Katibu Tawala kwa
kugusa makundi mbalimbali na kuibua changamoto katika ngazi ya
jamii" amesema.
Mratibu wa Uchaguzi Jiji la Mbeya Gregory Emmanuel amesema Jiji
limetulia na uchaguzi umekwenda vizuri kikubwa wanahimizwa
ushirikiano katika kuwafikia wananchi.
No comments:
Post a Comment