Thursday, November 14, 2024

WAMUOMBA MBUNGE KUKAMILIKA JENGO KITUO SHIKIZI


Wananchi wa kijiji cha Mpolo Wilaya Mbarali Mkoa wa Mbeya wameomba Mbunge wa Jimbo hilo, Bahati Ndingo kuwasaidia kukamilisha jengo la kituo cha elimu shikizi ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi.

Ombi hill wamelitoa jana Novemba 14, 2024 kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge huyo uliolenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Mkazi wa kijiji cha Mpola Shija Masanja amesema ukosefu wa shule shikizi umepelekea watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu.

Wakati huo huo wameomba kuboreshwa miundombinu ya barabara, umeme kijijini hapo ili kuwasaidia kuchochea shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wake Mbunge wa Mbarali Bahati Ndingo amehaidi kufanyia kazi maombi yao sambamba na ujenzi wa jengo la kituo shikizi kutokana na jitihada zilizofanywa na wananchi.

"Nimeona jitihada zenu kama wananchi niwahaidi kushughukia changamoto hizo sambamba na kuchangia Sh 600,000 kwa ajili ya kuweka kifusi kwenye eneo korofi la barabara ya Mpolo kwenda Ihanga .

Ndingo amesema marekebisho ya miundombinu ya barabara hiyo utasaidia wananchi kusafirisha mizigo kutoka sehemu moja kwenda maeneo mbalimbali wilayani humo.

Mbunge huyo pia amechangia Sh 250,000 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya michezo hususani jezi na mpira baada ya vijana  kuwasilisha ombi kwake.

No comments:

Post a Comment