Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) imetoa pikipiki 10 zikiwepo za matairi matatu (bajaji) mbili kwa umoja wa bajaji na bodaboda jiji la Mbeya kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali kuwezesha vijana kujiajiri
Meneja Masoko na Uendelezaji wa Benki ya PBZ Mohamed Ismail amesema jana Novemba 25, 2024 mara baada ya kumkabidhi Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackon kwenye maadhimisho ya miaka 15 ya umoja wa bajaji Jiji la Mbeya yaliyo fanyika viwanja vya Mwenge.
Ismail amesema kwa kutambua vijana ni chachu ya maendeleo na namna gani Mbunge wetu na Spika Dkt. Tulia Ackson anavyowekeza kusaidia vijana kujiajiri.
"Tunaendelea kukuunga mkono Dkt. Tulia kwani umekuwa chachu ya maendeleo na kuwakusanya vijana katika suala la kujiajiri na kutoa mikopo ya pikipiki na bajaji kupitia Taasisis ya Tulia Trust" amesema Ismail.
Aidha amewataka madereva bajaji na pikipiki kuchangamkia benki ya PBZ kuwekeza katika masuala ya bima kwa gharama nafuu ili kuepuka changamoto za matibabu zinazotokana na ajali za barabarani
Kwa upande wake Spika wake Bunge na Munge wake Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackon amesema vijana watumie vyombo hivyo kama ajira kamili kwani wameshuhudia maisha yao yanatoka sehemu moja kwenda nyingine.
"Nimeshuhudia mbali na kutimiza miaka 15 pia nimezindua jengo la ofisi ya bajaji Kanda ambayo itakuwa kitega uchumi nitumie fursa hiyo kuwapongeza sana" amesema Dkt. Tulia.
Dkt. Tulia ameishukuru Benki yaa PBZ kwa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kufungua tawi mkoani hapa hivyo ni fursa kwa madereva wa bodaboda na bajaji kuchangamkia fursa ya kuwekeza.
Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji la Mbeya Aliko Fwanda amesema wanashukuru kwa Connection za fursa zinazoletwa na Mbunge wao katika suala la kuhakikisha vijana wanajiajiri na kuacha kushinda mitaani.

No comments:
Post a Comment