Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mkoa wa Mbeya Bahati Ndingo amesema wamejipanga CCM kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024 na kuwataka wananchi kuendelea kukiamini.
Ndingo amesema jana Novemba 21, 2024 wakati wa uzinduzi wa kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo zilizo fanyika katika kata ya Ubaruku huku mgeni rasmi akiwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa.
"Tuna uhakika Mbarali kushinda kwa kura za kishindo uchaguzi wa serikali za mitaa wagomea tulio wasimamisha tuna imani nao kwa asilimia 100 na kwamba mitaa 53 watapita bila kupingwa baada ya upinzani kutosimamisha wagombea" amesema Ndingo.
Amefafanua mpaka sasa CCM wameweka wagombea mitaa 112 vitongoji 712 hivyo kwa takwimu hizo ushindi wa kishindo ni lazima.
Ndingo amewataka wananchi wa Jimbo la Mbarali kuunga mkono jitihada za serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kuendelea kuleta maendeleo na kutatua changamoto zilizopo.
"Rais anatambua changamoto zenu wanambarali uchaguzi huu msifanye makosa tunaendelea kuleta maendeleo ikiwepo kutatua migogoro iliyopo" amesema.
Awali akizungumza na wananchi Mchungaji Msigwa amewaonya kutothubutu kujiunga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na badala yake wachague viongozi wa CCM.
Amesema CCM chini ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan imeleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali za kiuchumi hususani kupunguza vifo vya Mama na mtoto kwa kusogeza huduma za afya karibu.
Wakati huo huo wananchi Jimbo la Mbarali wameeleza kuendelea kukiunga mkono na kumuelezea Mbunge wao Bahati Ndingo kuleta mageuzi kwa kipindi kichache tangu wamchague
Kwa upande wake aliyewahi kuwa Mbunge viti maalum Mkoa wa Mbeya Dkt. Mary Mwanjelwa amesema CCM iende na kasi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya 4R katika kujenga Demokrasia ya Maendeleo ya nchi.

No comments:
Post a Comment