Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Renatus Mchau ameahidi kujenga vituo vya maegesho ya bodaboda katika mji wa Tukuyu na vitongoji vyake ikiwa ni jitihada ya kuboresha mazingira ya usafirishaji wa abiria na mali zao.
Ahadi hii ameitoa katika kikao maalumu cha viongozi wa Bodaboda ambapo pamoja na viongozi wengine pia Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka jeshi la polisi kimeshiriki.
Amesema Bodaboda ni biashara halali kama zilivyo biashara nyingine hivyo kuna haja ya kuboresha mazingira yake ambapo mabanda maalumu ya maegesho yatajengwa. Zoezi hili linalotarajia kuanza katika mwaka wa fedha 2024/25.
Kwa upande wa Bodaboda wameahidi kuendelea kutoa
ushirikiano kwa Taasisi zote za serikali ikiwemo LATRA na Jeshi la
Polisi pamoja na kulipa tozo zote zilizopo kwa mjibu wa sheria.
Bodaboda
wameomba kuendelea kushirikishwa kila inapohitajika ikiwa ni hatua ya
kuunga mkono jitihada ya Serikali ambayo imejikita kuwaletea maendeleo
wananchi hasa wa tabaka la chini.
No comments:
Post a Comment