Friday, July 12, 2024

NDELE MWASELELA AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO MBEYA DC

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (MNEC) Ndele Mwaselela amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 16 bora zinazoshiriki ligi ya Mama Samia Mshikamano Cup inayoendelea katika viunga vya wilaya hiyo, vifaa hivyo ni pamoja na mipira na jezi.

Mwaselela amekabidhi vifaa hivyo vya michezo kwa timu 16 Julai 11, 2024 katika ofisi za CCM mkoa wa Mbeya.

Hata hivyo Mwaselela amesema kuwa michezo ikawe chombo cha kuzitafsiri 4R za Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuelezwa kwa mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Samia katika kipindi cha uongozi wake.

DKT. TULIA NA RAIS WA URUSI WAJADILI NAMNA BORA YA KUIMARISHA AMANI DUNIANI

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson,  amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi, Vladimir Putin Jijini St. Petersburg nchini Urusi leo Julai 12, 2024 ambapo katika mazungumzo yao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha amani Duniani.

“Kabla ya kuzungumza naye tayari tulishazungumza na Maspika wa nchi zote hizo mbili na sisi kama Umoja wa Mabunge Duniani tumezungumza naye kama Kiongozi wa nchi katika sura ambayo tunaweza kuziweka pamoja nchi zote mbili na tutarajie kwamba IPU itatengeneza fursa ya Mabunge ya pande zote ili kuweza kuzungumzia amani katika maeneo yao ya utawala” amesema Dkt. Tulia.


TULIA TRUST YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE MASHULENI

Taasisi ya Tulia Trust imeanza zoezi la ugawaji na utoaji elimu ya matumizi yaTaulo za kike wenye mahitaji maalumu kwa shule za sekondari kata 36 za Jiji la Mbeya.

Lengo ni kuwezesha wanafunzi wa kike kutoka mazingira magumu kuweza kupata elimu bora pasipo kuwa na changamoto zinazotokana na hedhi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo, Meneja wa Taasisi ya Tulia Trust, Jackline Boaz amesema watazifikia kata tano Mbeya mjini kwa kutoa taulo za kike.

Amesema zoezi hilo litanufaisha kwa wanafunzi wa kike kutoka kaya maskini ambao wamepewa taulo za kike 550 sambamba na viatu pea 50.

Thursday, July 11, 2024

MAFUNZO YA MFUMO WA GAMIS YATOLEWA KWA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA


Menejimenti ya hospitali, wakiwemo watendaji kutoka Idara  mbalimbali za Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) leo Julai 11, 2024 wamepewa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Mali za Serikali (Government Assets Management Information System (GAMIS) ili kuwawezesha kuingiza na kuhuisha taarifa za mali za taasisi kwenye mfumo kwa wakati.

Mafunzo hayo yametolewa na wakufunzi kutoka Wizara ya Fedha Said Mtatura na Simon Njoka ambaye pia ni msimamizi wa mali za Serikali Mkoa wa Mbeya na Songwe na kueleza kuwa mafunzo hayo ni wezeshi kwa maafisa usimamizi wa mali za Serikali hususani maafisa wapya kwa lengo la kuwajengea uwezo kwenye matumizi ya moduli zilizopo kwenye Mfumo wa GAMIS.

DKT. TULIA AJITOLEA KUMSOMESHA MTOTO ALIESHINDWA KUENDELEA NA MASOMO KWA KUKOSA MAHITAJI

Kijana Richard (kushoto) akiagana na Mratibu wa Tulia Trust Addy Kalinjila Mara baada ya kumkabidhi kwa uongozi wa shule ya wavulana Uwata.

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU) Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson amejitolea kukuendeleza elimu ya kidato cha tano na sita Yatima Shadrack Mwaisela (17) aliyekwama kuendelea na masomo kwa kukosa mahitaji.

Kijana Richard aliyekuwa akiishi na bibi yake mkazi wa kijiji cha Kisondela Wilaya ya Rungwe  amekabidhiwa leo Alhamisi  kwa uongozi wa Shule ya Sekondari ya wavulana Uwata kupitia Taasisi ya Tulia Trust.

Akizungumza mara baada ya kumpokea Mwanafunzi huyo Makamu Mkuu wa Shule Wavulana  Uwata, Marco Mwakanyamale amemshukuru Dkt. Tulia kwa moyo wa kumuendeleza  kielimu kufatiatia kutoka katika mazingira magumu.

RUNGWE KUTUMIA NGOMA ZA ASILI KUTANGAZA UTALII

Mbunge wa Jimbo la Rungwe, Athon Mwantona ameanzisha mashindano ya ngoma za asili,nyimbo za injili na mashindano ya mpira wa miguu kwa lengo la kutangaza fursa za uwekezaji kwenye utalii.

 Katibu wa Mbunge, Gabriel Mwakagenda amesema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mipango mikakati ya kuitangaza Wilaya ya Rungwe na kuvutia uwekezaji.

Mwakagenda amesema Wilaya ya Rungwe ina vivutio vingi vya utalii ambavyo vikitumika vinatengeneza fursa za kiuchumi kwa vijana na hata mapato kwa serikali.

Wednesday, July 10, 2024

BILION 5.3 KUJENGA SOKO LA KISASA LA NDIZI RUNGWE

Serikali  Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya inatarajia kutumia zaidi ya Sh 5.3 bilioni kwa ajili ya  ujenzi wa soko la kisasa la mazao ikiwepo ndizi na parachichi.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kuwepo kwa changamoto ya masoko ya uhakika hali iliyopelekea wakulima kushindwa kunufaika na uzalishaji

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Julai 10, 2024 na katibu wa Mbunge wa Jimbo la Rungwe, Gabriel Mwakagenda kwa niaba ya Mbunge Athon Mwakagenda.

Amesema kuwa mradi huo wa soko la kisasa itakuwepo miundombinu mbalimbali ikiwepo migahawa,maegesho,Taasisi za kifedha za kitanzania na kigeni na huduma nyinginezo.

Tuesday, July 9, 2024

DC: MALISA ATAKA WATU WENYE UALBINO WALINDWE


Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa ameagiza viongozi wa serikali za mitaa kuchukua hatua ya kuelimisha jamii kuwalinda watu wenye ualbino.

Malisa amesema leo Jumatatu Julai 8, 2024 kwenye maadhimisho ya siku ya afya ya ngozi duniani iliyofanyika kitaifa Mkoa wa Mbeya na kuratibiwa na Shirika la Standing Voice kwa kushirikiana na Hosptali ya Rufaa ya Mkoa.

Amesema sasa imefika mwisho kwa watu ambao wanatafuta mali kwa kuwaua albino na kisha kwenda kuuza viungo vyao watakao bainika sheria itachukua mkondo wake.

Friday, July 5, 2024

DKT. TULIA AMGUSA YATIMA KUCHANGIA MAHITAJI YA SHULE

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU ) Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson ametoa zaidi ya Sh 500,000 kwa ajili ya mahitaji ya shule kwa  mtoto yatima aliyechaguliwa kujiunga kidato cha tano Shule ya Sekondari Isongole Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.

Fedha hizo zimekabidhiwa leo Ijumaa Julai 5, 2024 na Ofisa habari na Mawasilino wa Taasisi ya Tulia Trust Addy Kalinjila kwa mlemavu Richard Mwaisela (18) ambaye ni yatima anayelelewa na bibi yake  ambaye alikwama kuendelea na masomo kwa kukosa mahitaji.

"Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust ameguswa kumsaidia Richard aweze kutimiza ndoto yake ya kupata elimu kwani bibi yake mkazi wa kijiji cha Mpuga kata ya Kisondela  alikosa uwezo wa kumsaidia baada ya kufaulu kujiunga idato cha tano Shule ya Sekondari ya Isongole na kushindwa  kuanza masomo " amesema Kalinjila.

Kalinjila amesema kuwa kama Taasisi wataendelea kuigusa jamii yenye mahitaji kwa kuchangia sekta ya elimu, afya na kuwezesha jamii isiyojiweza.

Kwa upande wake kijana Richard amemshukuru Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwa kumuwezesha kupata mahitaji na kuhaidi kusoma kwa bidhii ili kutimiza ndoto zake za kupata elimu.

Thursday, July 4, 2024

ALIYECHOMA PICHA YA RAIS AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI


Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya imemtia hatiani ni kumhukumu kutumikia kifungo cha miaka miwili Shadrack Chaula (24) au kulipa faini ya Shilingi milioni tano.

Shadrack ametiwa hatiani kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Tik Tok kinyume cha  kifungu cha sheria 16 ya mtandao ya kijamii.

Hukumu hiyo imesomwa leo Julai 4, 2024 na Hakimu mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe, Shamla Shehagiro baada ya mawakili wawili wa serikali, Rosemary Mginyi na Veronica Mtafya kutoa ushahidi mahakamani hapo.

Imeelezwa mahakamani hapo mtuhumiwa alitenda kosa hilo June 22 mwaka huu katika eneo la Ntokela wilaya ya Rungwe kwa kusambaza video yenye taarifa za uongo kinyume cha kifungu cha sheria 16 ya makosa ya mitandao.


TAASISI YA TULIA TRUST IMETOA BANDO TISA ZA BATI UJENZI WA UKUMBI

Taasisis ya Tulia Trust umekabidhi msaada wa mabati bando tisa za bati kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa  ofisi ya chama cha Mapinduzi shina namba nane kata ya Iyela Jijini hapa.

Msaada huo wa Mabati umetolewa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge (IPU) Dkt. Tulia Ackso Ackson, Steven Chambanenge.

Amesema kuwa Dkt. Tulia amekuwa na mapenzi mema kwa wanambeya na kuwataka asifanye makosa unapofika wakati kwa kupiga kura za kishindo kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Mbunge wao Dkt. Tulia Ackson.


Kwa upande wake Mjumbe wa shina namba nane, Gaporic Lwibha amesema anamshukuru Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa kuchangia ujenzi wa ukumbi huo.

"Ndugu zangu tulitumia muda mfupi sana kuomba lakini leo hii tumekabidhiwa, naomba Katibu wa Mbunge nifikishie salama za shukrani zetu kuna majibu yake 2025 kwake Rais Samia Suluhu Hassan" amesema.

Monday, July 1, 2024

KATA 13 JIJI LA MBEYA ZANUFAIKA NA MICHE YA PARACHICHI 1,120 BURE

Miche zaidi ya 1,120 ya matunda aina ya parachichi kwa wananchi katika kata 13 jijini Mbeya kati ya 36 zitakazo nufaika kwa lengo la uzalishaji wa kiuchumi na kutunza mazingira.

Miche hiyo imetolewa na Taasisi ya Tulia Trust kupitia Mkurugenzi wake Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson ikiwa ni mikakati yake ya kuifanya Mbeya kuwa ya kijani.

Akikabidhi miche hiyo kwa wananchi, watendaji wa Serikali na viongozi wa chama Mratibu wa zoezi hilo na Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi hiyo, Addy Kalinjila amesema hilo ni zoezi endelevu na miche hiyo inatolewa bure.

Tuesday, June 25, 2024

CHUNYA YAPAMBANA KUKAMILISHA UWANJA KABLA YA KUANZA MSIMU MPYA WA LIGI KUU 2024/ 2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Tamim Kambona amesema Halmashauri yake imetenga shilingi milioni mia mbili kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa michezo uliopo Kata ya Mbugani unaomilikiwa na Halmashauri ili ukamilike kabla ya kuanza kwa ligi Kuu mwaka 2024/ 2025 utakaotumiwa na timu ya Ken Gold iliyopanda daraja msimu huu.

Akizungumza na MBPC blog Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya amesema mbali ya kutenga fedha hiyo kupitia mapato yake ya ndani pia imeunda kamati ya wadau inayoongozwa na Ayoub Omary.

Kambona amesema sanjari na mipango ya kamati Halmashauri inatarajia kutenga fedha nyingi zaidi mwaka ujao wa fedha ambapo uwanja huo wa kisasa utatandikwa zuria kwa ajili ya mpira wa miguu.