Friday, February 21, 2025

HASHIM RUNGWE KUFANYA MKUTANO WA HADHARA MBEYA, UBWABWA BURE

Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kinatarajia kufanya Mkutano wa hadhara Februari 22, 2025 Mwanjelwa Jijini Mbeya mkutano utakaoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Hashim Rungwe.

WATU WATANO WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UPATU MTANDAONI

 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya linawashikilia watu wa tano wa kampuni ya LBL kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya upatu mtandaoni bila kuwa na kibali na kuwashawishi wateja kulipa fedha.

KENGOLD vs KMC, TIMU ZAELEZA JINSI ZILIVYOJIPANGA KUONDOKA NA ALAMA TATU

 

Kuelekea mechi ya KenGold dhidi ya KMC itakayochezwa kesho Februari 22, 2025 saa nane mchana katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya makocha wa timu zote wameeleza namna walivyojiandaa kuondoka na alama tatu muhimu katika mchezo huo.

Tuesday, February 18, 2025

WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2025


Wananchi wa jimbo la Mbeya vijijini wametakiwa kujipanga kikamilifu kushiriki katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025 ili kuchagua viongozi wataotekeleza miradi ya maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya vijijini Oran Njeza ametoa kauli hiyo jana Februari 18, 2025 wakati wa hafla ya kuwapongeza wenyeviti wa serikali za mitaa na vitongoji waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa mwaka 2024.

Njeza, amepokelewa na maelfu ya wananchi wa Kata ya Isuto jimboni kwake amesema anawashukuru wananchi kwa kuwaamini viongozi hao kwa wakati mwingine ili kuunga mkono juhudi za serikali kuwaletea maendeleo.

 

Monday, February 17, 2025

CHIEF GODLOVE ADHAMINI MASHINDANO YA UMITASHUMTA KYELA

Timu 120 kutoka Shule mbalimbali za msingi wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya zimeshiriki Mashindano ya Michezo ya Taaluma Tanzania (UMITASHUMTA) yaliyoanza kutimua kivumbi jana kwenye viwanja tofauti.

Mdhamini mkuu wa mashindano hayo, mdau wa michezo nchini, Chief Godlove Mwakibete ambaye mbali na udhamini amechangia mahitaji mbalimbali na zawadi kwa washindi.

Akizungumza na waandishi wa habari, amesema ameguswa kudhamini lengo ni kuunga mkono juhudi za serikali kuhamasisha michezo na kuibua vipaji vya vijana mashuleni na kuviendeleza.

"Vijana tunahitaji kuunga mkono serikali kuwekeza katika michezo kwa kuibua vipaji vya wanafunzi na kuvikuza kupitia michuano mbalimbali kwa kutambua michezo nia afya, michezo ni fursa ya ajira" amesema Mwakibete.

Thursday, February 13, 2025

NJEZA: BUNGE LIMESHAURI UKUSANYAJI KODI ZA MAJENGO UREJESHWE SERIKALI ZA MITAA

Mbunge wa Jimbo la Mbeya vijiji Oran Njeza ameishauri serikali kuondoa makusanyo ya kodi za majengo kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenda serikali za mitaa.

Njeza amesema Bunge limeshauri kuhakikisha kiwango cha asilimia 20 ya mapato ya kodi za majengo zielekezwe kwenye Halmashauri kwa wakati.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya kamati ya bunge kwa mwaka wa fedha 2024.

Amesema katika mwaka fedha 2024/2025 serikali iongeze kiwango kinacho rejeshwa katika halmashauri kutoka asilimia 20 mpaka 50 ili kuharakisha zoezi la uthamishaji wa majengo na kurejesha asilimia 20.

Sambamba na hilo Mbunge Njeza amesema bunge limeshauri kuboreshwe mfumo wa tausi katika ukusanyaji wa mapato ya majengo sambamba na kuongeza idadi ya wataalamu ili kurahisisha utekelezaji.

Taarifa hiyo imeungwa mkono na wananchi huku wakieleza itawezesha kulipa kwa hiyari kodi ya majengo tofauti na makusanyo kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA).

Tuesday, February 4, 2025

DC MALISA AHIMIZA WANANCHI KUJENGA UTAMADUNI WA KUPIMA SARATANI

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya ili kukabiliana na ugonjwa saratani, huku takwimu zikionyesha watu 500 wamepatiwa huduma baada ya kubainika.

Malisa amesema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera kwenye Maadhimisho ya siku Saratani Duniani yaliyofanyika leo Jumanne Februari 4, 2024 katika Hosptali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH).

"Niwasisitize wananchi kupima afya mara kwa mara tunaona takwimu zinaonyesha watu 500 wamegundulika kuwa na saratani hususani kwa wanawake na wanaume" amesema Malisa.