Thursday, March 20, 2025

ENG. MAHUNDI AANZA ZIARA KUKAGUA HUDUMA ZA MAWASILIANO MPAKA WA KASUMULU NA TUNDUMA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amewasili katika ofisi za Mkoa wa Mbeya na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Juma Homera, leo Machi 20, 2025.

Akimkaribisha Naibu Waziri Mahundi, Mkuu wa Mkoa, Dkt. Homera, ameipongeza wizara kwa kazi nzuri inayofanya katika kuboresha hali ya mawasiliano mkoani humo.

Dkt. Homera ameomba Wizara kuhakikisha maeneo ya Utalii yanakuwa na mawasiliano bora zaidi ili kuchochea Sekta ya Utalii, pamoja na kuendelea kuboresha huduma za mawasiliano katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo, ikiwemo Kyela.

Kwa upande wake, Mhandisi Mahundi amesema ziara yake inalenga kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo ya mpakani ya Kasumulu uliopo Mkoa wa Mbeya na Tunduma, mkoani Songwe, ambapo wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kupokea taarifa kutoka mitandao ya nchi jirani badala ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment