Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini  Oran M. Njeza, amezitembele na kutoa mkono wa pole kwa familia za watu 29 waliofariki na majeruhi  wa ajali.
Ajali hiyo ilitokea  Juni 7, 2025 katika mtelemko mkali wa mlima Iwambi Wilaya ya Mbeya, baada ya ya lori lilokuwa limebeba shehena za unga kugonga  magari mawili yakiwepo ya abiria.
Katika ajali hiyo watu 28 walipoteza maisha papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa na kukimbizwa katika Hosptali Teule ya Ifisi Wilaya ya Mbeya.

Amesema baada ya kuwasilisha hoja za kamati bungeni jijini  Dodoma Juni 16, 2025 amelazimika kurejea jimboni kutoa mkono wa pole kwa familia zilizo poteza wapendwa wao na kuwajulia hali  majeruhi wote wa ajali hiyo.



No comments:
Post a Comment