Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa, amehamasisha wananchi kutumia fursa ya ujio wa Madaktari Bingwa Bobezi wa Dkt Samia kufanyiwa vipimo vya uchunguzi wa magonjwa.
Kambi ya madaktari bingwa bobezi imeanza leo Mei 5 mpaka Mei 9, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya (Mbeya RRH) kwa muda wa siku tano.
Amesema huduma hizo zitawanufaisha wananchi kutoka mikoa Nyanda za Juu Kusini ikiwepo Mbeya, Ruvuma Songwe, Songea Njombe.
Awali mkazi wa Njombe Vaileth Kwese,amesema kitendo cha serikali kuwafikishia huduma kimewapunguzia gharama za kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu.
Akizungumza na maelfu ya wananchi kwenye uzinduzi wa kambi hiyo, Malisa amesema ni matokeo ya uwekezaji wa Serikali ya awamu ya sita ikiwepo ununua vifaa na kuendeleza wataalamu wa kada za afya.
"Niwashukuru wote mliojitokeza kupata huduma hizi, lakini mkawe mabalozi wazuri kwa wananchi wengi kueleza ujio madaktari bingwa bobezi wa magonjwa mbalimbali.
Malisa amewataka wakisubiri siku ya mwisho ambapo kutakuwa na wageni kutoka mikoa mbalimbali.
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri Hosptali ya Mkoa Dkt. Julius Kaijage, amesema wana kila sababu ya kuishukuru serikali kwa kusogeza huduma ambazo walikuwa wakutumia gharama kubwa kuzifuata.

Mganga Mfawidhi, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya Dkt. Abdallah Mmbaga amesema kambi hiyo madaktari bingwa na bingwa bobezi itadumu kwa siku tano na kueleza mkakati wao wa kuwapatia ushirikiano mkubwa kwa kipindi hicho.
Miongoni mwa huduma za kibingwa zitakazo tolewa kwa wananchi wa ni pamoja na Ubingwa katika Magonjwa ya Watoto, Wanawake na Uzazi, Magonjwa ya Ndani.

No comments:
Post a Comment