Wanafunzi watano wa Sekondari ya Chalangwa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya
wamefariki kwa kugongwa na basi lenye namba za usajili namba T 194 DCE
aina ya YUTONG linalomilikwa na Kampuni ya Safina linalofanya safari
zake Lualaje Mbeya Julai 26, 2025 majira ya saa 11:30 alfajiri barabara
kuu ya Chunya Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Wilbert Siwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo wanafunzi watano wamefariki papo hapo na majeruhi tisa wamepokelewa Kituo cha Afya Chalangwa.
Siwa amesema mara baada ya tukio dereva wa basi hilo alitoroka na juhudi za kumtafuta zinaendelea ambapo ametoa wito kwa madereva kuwa waangalifu wawapo barabarani na chanzo kikitajwa ni mwendo kasi na uzembe wa dereva.

Kufuatia ajali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Mbarack Alhaj Batenga amepiga marufuku kwa Shule au vikundi vya michezo kukimbia barabarani badala yake watumie viwanja vya michezo vilivyotengwa katika kila shule kufanya mazoezi.
Aidha Batenga amesema Serikali itagharamia mazishi na matibabu kwa majeruhi wote wa ajali.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa pole ya ubani wa shilingi laki tano kwa wafiwa waliokumbwa na msiba huo mzito.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Chalangwa Dkt. Ernest Fraiton amesema wamepokea miili ya wanafunzi watano msichana mmoja na wavulana wanne na msichana mmoja wakiwa wamefariki pia majeruhi tisa ambapo kati yao walikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Chunya.
Solomon Eliah Mkuu wa Shule ya Sekondari Chalangwa amesema shule imekuwa na utaratibu wa kila jumamosi kwa wanafunzi kukimbia kwa ajili ya kuwapa utimamu wa mwili na wakati wa mazoezi hayo walimu wawili walikuwa wakiwaongoza wanafunzi hao wa bweni ambao idadi yao haikufahamika mara moja.
Bethania Charles ni mwanafunzi wa kidato cha pili ambaye amevunjika mkono amesema mapema walipokuwa wanageuza eneo la Itumbakutoka Chalangwa Sekondari walishangaa basi hilo likiwagonga kwa nyuma.

No comments:
Post a Comment