Ameongeza kuwa msaada huo ni matokeo ya ushirikiano wanaopatiwa hivyo amewataka watumiaji wa vifaa hivyo kuvihifadhi vizuri ili viendelee kufanya kazi kwa ubora.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dkt. Uwesu Mchepange, ametoa shukrani kwa wadau wa maendeleo, hususan Shirika la KCOO, kwa msaada wa vifaa vya uchunguzi na matibabu venye thamani ya zaidi ya milioni 100 walivyopatiwa.
Ameongeza
kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muafaka, kwani utaongeza kasi ya
utoaji huduma na kupunguza muda wa magonjwa kufuata huduma. Vifaa hivyo
ni pamoja na mashine za upasuaji wa macho kwa watoto, ultrasound ya
kupima macho, na vifaa vya macho saidizi, vyote vililenga kuboresha
huduma ya matibabu ya macho kwa watoto.
Kwa upande wake Dkt.
Barnabasi Mshangila, Daktari Bingwa Bobezi wa macho kwa watoto,
amemshukuru Uongozi wa hospitali kwa ushirikiano mkubwa na ameeleza kuwa
msaada huu utasaidia kuboresha huduma za matibabu ya macho kwa watoto,
na kwamba hakutakuwa na haja yarufaa kupeleka watoto kupatiwamatibabu
ya kibingwa sehemu nyingine, kwani huduma zitapatikana kwa karibu zaidi.
Pia, ameahidi kuwa vifaa hivyo vitatunzwa kwa umakini ili viweze kudumu
na kutoa huduma kwa muda mrefu, na kuimarisha ustawi wa afya ya macho
kwa watoto watakaofika kwaajili ya huduma.
No comments:
Post a Comment