Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Malisa amezindua mpango mkakati wa Dira ya miaka mitano ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kumkabidhi rasmi Meya Jiji la Mbeya Dour Mohamed Issa
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jumatano Juni 11, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa mkapa jijini hapa, ikiwa ni uzinduzi wa mpango mkakati wa dira ya miaka mitano ya 2025/26 mpaka 2029/2039 kwa halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Dira hiyo imebeba vipaumbele 29 ikiwepo masuala ya elimu, afya maboresho ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ujenzi wa bandari ya nchi kavu, sekta ya afya na elimu na mengineyo mengi.
Malisa amepongeza wadau walio fanikisha Halmashauri ya Jiji kutekeleza mkakati, huku akitaka kuweka kipaumbele katika uboreshwaji miundombunu ya masoko ili wafanya biashara waweze kufanya kazi masaa 24.
Katika hatua nyingine Malisa amesema katika ujenzi wa kituo cha watoto mazingira magumu waweke kipaumbele cha kuwajengea uwezo.
"Wajengewe uwezo ili wasirejee mitaani lengo ni kuona wanadhibitiwa na kupata ujuzi kwa kuzingatia Mkoa wa Mbeya kuwa katikati ya mikoa saba nchini" amesema.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Jiji la Mbeya Dour Mohammed Issa amesema mpango mkakati huo unakwenda kuboresha Jiji la Mbeya.
"Madiwani tumeshiriki kikamilifu katika kufikia mpango mkakati huo wa dira ya miaka mitano yani 2029/2039 lakini nishukuru wadau walichangia hususani katika suala la lishe bora mashuleni" amesema.
No comments:
Post a Comment