Tuesday, February 18, 2025

WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2025


Wananchi wa jimbo la Mbeya vijijini wametakiwa kujipanga kikamilifu kushiriki katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025 ili kuchagua viongozi wataotekeleza miradi ya maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya vijijini Oran Njeza ametoa kauli hiyo jana Februari 18, 2025 wakati wa hafla ya kuwapongeza wenyeviti wa serikali za mitaa na vitongoji waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa mwaka 2024.

Njeza, amepokelewa na maelfu ya wananchi wa Kata ya Isuto jimboni kwake amesema anawashukuru wananchi kwa kuwaamini viongozi hao kwa wakati mwingine ili kuunga mkono juhudi za serikali kuwaletea maendeleo.

 

Amesema serikali ya awamu ya sita imetekeleza ilani ya uchaguzi 2020 katika kuleta maendeleo katika  nyanja mbalimbali hususani sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara.

"Wananchi tunaona Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa zawadi yake pekee ni kumpa kura za kishindo katika uchaguzi Mkuu Oktoba 2025" amesema Njeza.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Mkoa wa Mbeya Antony Mwaselela amehimiza wenyeviti walio chaguliwa kuwa na umoja na mshikamano ili kwenda kutatua kero za wananchi.


No comments:

Post a Comment