Pamoja na kuthibitisha kushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka huu, Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimependekeza na kuishauri Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi baadhi ya mambo kufanyiwa marekebisho kabla ya zoezi hilo.
Tanzania inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 25 mwaka huu kuwapata madiwani, wabunge na Rais, huku Chama hicho kikitarajia kusimamisha wagombea katika nafasi zote.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Aprili 7, 2025, Katibu Mwenezi wa Chama hicho Taifa, Ipyana Njiku amesema katika kikao cha Halmashauri kuu ya Chama hicho Februari 19, 2025 kiliazimia kushiriki uchaguzi huo katika nafasi zote na kutoa mwelekeo wa nchi kwa miaka mitano ijayo.

Amesema pamoja na maamuzi hayo, lakini wamependekeza na kuishauri Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, kufanya mabadiliko kwa wasimamizi wa uchaguzi badala ya makamishna na wakurugenzi, wananchi waombe nafasi hizo na watakaokidhi wapewe kazi hiyo.
"Wakurugenzi wasiwe wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo kwakuwa hao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wasimamizi wa uchaguzi kwenye vituo wasipangwe watumishi wa Umma na mawakala wa vyama wasipewe usumbufu kama ambavyo imejitokeza huko nyuma" amesema Njiku.
Katibu huyo amewaomba wananchi kujiandaa na kushiriki vyema uchaguzi huo huku akiwaomba vijana wenye sifa kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi huo.
Amefafanua kuwa Chauma hakishirikiani wala kufungamana na chama chochote cha siasa akieleza kuwa hawaelekezwi au kuagizwa na mtu yeyote kufanya uamuzi wowote kwani ni chama chenye katiba na usajili wake binafsi.
"Kimekuwa na mnong'ono kwamba tunashirikiana na chama fulani na ni mawakala, huu ni uongo na uzushi, sisi tunafanya kulingana na katiba yetu kwakuwa usajili unatambulika kwa msajili" amesema Katibu huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Mbeya.
Ameongeza kuwa iwapo Chama hicho kitashinda dora, hoja yao ni kutoa elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi chuo na sera ya 'ubwabwa' itakuwa katika meneo yote ikiwamo Hospitalini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vijana wa Chama hicho mkoani humo, Lusako Mwakilumwa amewaomba vijana, makada wa vyama vya siasa na wananchi ambao wanahitaji nafasi za uongozi kujiunga na chama hicho ili kukipa nguvu kuelekea uchaguzi mkuu.
"Wapo makada wa vyama vya upinzani ambao wanateseka kwenye vyama vyao wakihitaji nafasi za uongozi, niwaombe kuanzia vijana wenzangu na wananchi kwa ujumla waje kutimiza ndoto zao huku katika uchaguzi mkuu" amesema Mwakilumwa.
Mchambuzi na mlezi wa vyama vya siasa mkoani Mbeya, Chifu Prince Mwaihojo ameviomba vyama vyote vya siasa nchini kushiriki uchaguzi mkuu kwa maslahi ya nchi akieleza kuwa misimamo ya Chama chochote kutoshiriki kinaweza kupotea.
"Chama kimoja hakiwezi kuzuia uchaguzi, fujo za kwenye siasa zipo duniani kote, kikubwa ni kila mmoja kujipanga kulinda kura zake, sisi machifu tunajivunia watu tulionao" amesema Mwaihojo.
"Hakuna timu inaweza kufanya maandalizi na siku ya mechi wasicheze, niwaombe Chadema warudi nyuma na warudi kujiuliza hoja yao kwa wananchi" amesema mchambuzi huyo.

No comments:
Post a Comment