Thursday, November 30, 2023
HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE KUJENGA MAEGESHO YA BODABODA
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Renatus Mchau ameahidi kujenga vituo vya maegesho ya bodaboda katika mji wa Tukuyu na vitongoji vyake ikiwa ni jitihada ya kuboresha mazingira ya usafirishaji wa abiria na mali zao.
Ahadi hii ameitoa katika kikao maalumu cha viongozi wa Bodaboda ambapo pamoja na viongozi wengine pia Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka jeshi la polisi kimeshiriki.
Thursday, November 16, 2023
WAWEKAZAJI WA UTALII MKOA WA TANGA WATAKIWA KUJIANDAA NA MKUTANO WA WADAU WA MAZAO YA NYUKI DUNIANI 2027.
Wadau wa sekta ya utalii, sekta ya ufugaji nyuki na mazao yatokanayo na Nyuki wametakiwa kujiandaa na mkutano mkubwa wa wadau wa ufugaji nyuki na wazalishaji wa mazao yatokanayo na ufugaji nyuki utakao fanyika Jijiji Arusha mwaka 2027.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula amesema hayo alipokuwa anatoa salamu za Wizara kwenye Kongamano la Uwekezaji, Biashara na Utalii na Uzinduzi wa Mwongozo wa uwekezaji Mkoa wa Tanga.
Mh. Kitandula alisema kwamba kupitia
mada mbalimbali zitakazowasilishwa katika kongamano na maonesho
yanayoendelea katika mabanda, anaamini kuwa wawekezaji wengi watavutiwa
kuja kuwekeza katika Mkoa wa Tanga kwani fursa nyingi zitaelezwa hapa
zikiwemo za sekta ya Utalii.
Monday, May 8, 2023
WIZARA YA KILIMO YATENGA BIL. 970
Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Mohammed Bashe (Mb)
Wizara ya Kilimo leo imeomba Bunge liidhinishe jumla ya Shilingi 970,785,619,000 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha 2023/ 2024.
Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake bungeni mjini Dodoma leo, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema, utekelezaji wa Mpango wa Bajeti wa Mwaka 2023/2024 umejikita katika maeneo matano ya kipaumbele na mikakati ya utekelezaji 26.
“Shughuli za kilimo hapa nchini ni muhimu kwa maisha na ustawi wa watu na uchumi wetu. Kimsingi, kilimo ni nyenzo muhimu katika mapambano dhidi ya umaskini wa kipato na umaskini wa chakula.
“Kilimo kinapanua fursa za ajira kwa kushirikisha wananchi wengi katika mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo na hususan biashara ya mazao ya kilimo ndani ya nchi na kimataifa,” amesema Waziri Bashe.
Wednesday, November 3, 2021
KESI YA MBOWE YAAHIRISHWA, SHAHIDI APATWA NA TATIZO LA KIAFYA
Shahidi wa sita katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alitarajiwa kuanza kutoa ushahidi leo Jumatano Novemba 3, 2021 katika Mahakama Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Wakili wa Serikali Mwandamizi Robert Kidando, ameiomba Mahakama iahirishe kesi mpaka kesho kwa kuwa shahidi wao amepata tatizo la kiafya.
“Shauri linakuja kwa ajili ya kusikilizwa. mpaka jana kuna shahidi ambaye tulikuwa tumepanga kuendelea naye lakini amepata tatizo la kiafya. Hivyo tunaomba ahirisho mpaka kesho tutakapoweza kuendelea. Suala hili liko nje ya uwezo wetu,” amesema Kidando.
Kwa Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Peter Kibatala wamekubaliana na ombi hilo, lakini wakitaka upande wa mashtaka kuhakikisha wanaleta shahidi.
“Kwa kufuata amri ya Mahakama ya jana sisi tulikuwa tumejiandaa lakini kwa kuwa mambo yako hivi hatuna namna ila tunaomba tu wenzetu wajitahidi kesho tarehe 4 tuweze kuendelea,” amesema Kibatala.
Jaji Joachim Tiganga ameahirisha kesi hiyo hadi Kesho Alhamisi Novemba 4, 2021.
“Kufuatia maombi ambayo yameletwa na wakili Serikali kwamba shahidi waliyekuwa wamemwandaa amefika mahali hawezi kuja kutoa ushahidi kwa sababu zilizoelezwa za kiafya na kwa kuzingatia kuwa upande wa utetezi haukupinga basi maombi haya yanakubaliwa na shauri hili linaahirishwa hadi kesho.
“Upande wa mashtaka mnakumbushwa kuanda mashahidi ili tuweze kuendelea. Washtakiwa mtaendelea kuwa chini ya uangalizi wa Magereza,” ameeleza Jaji Tiganga.
Mbowe anakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kupanga kutekeleza ugaidi. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfan Bwire Hassan (mshtakiwa wa kwanza), Adamu Hassan Kasekwa maarufu Adamoo na Mohamed Abdillahi Ling’wenya.
Monday, November 1, 2021
MAADHIMISHO YA WIKI YA MSAADA WA SHERIA 2021 KUFANYIKA KITAIFA MKOANI MBEYA
| Mh. Juma Homera, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. |
Na Keneth Mwakandyali.
Wananchi mkoani wa Mbeya wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutumia fursa
ya Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Sheria inayofanyika kitaifa mkoani
hapa kuanzia Novemba 01 hadi Novemba 12 katika viwanja vya Ruanda
Nzovwe.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera
leo Novemba alipokua akitoa akizungumza na waandishi wa Habari ambapo
amewataka wananchi kuchangamkia fursa hii ili kuweza kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili.
Saturday, August 21, 2021
TANLAP YAWANOA WANAHABARI MBEYA
Mtandao wa watoa msaada wa sheria Tanzania (TANLAP) umeendesha mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoani Mbeya ili kuwaongezea uelewa juu ya umuhimu wa kuzingatia sheria inayosimamia utoaji wa huduma ya habari katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Mafunzo hayo yamefanyika Agosti 20 mwaka huu yakihusisha watendaji mbalimbali kutoka taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msaada wa kisheria ijulikanayo kama SAUTI YA HAKI.
Saturday, May 22, 2021
WAHITIMU KIDATO CHA SITA 2021 WAITWA NA JKT
Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2021 wametakiwa kuhudhuria mafunzo kwa mujibu wa sheria katika kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walizopangiwa kuanzia Juni Mosi hadi 10, 2021.
Hayo yamesemwa jana Jumamosi Mei 22, 2021 na Kaimu mkuu wa utawala wa JKT, Kanali Hassan Mabena huku akizitaja kambi hizo kuwa ni Rwamkoma Mara, Msange Tabora, Ruvu Pwani, Mpwapwa, Makutupora Dodoma, Mafinga Iringa, Mlale, Itaka Songwe, Luwa, Milundikwa Rukwa, Nachingwea Lindi na Kibiti Pwani.
Kambi nyingine ni Oljoro JKT Arusha, Mgambo, Maramba Tanga, Makuyuni Arusha, Bulombora na Mtabila Kigoma.
TULIA TRUST YASAIDIA UJENZI WA MATUNDU YA VYOO SHULE YA MSINGI ILOMBA
Sunday, May 9, 2021
DKT. TULIA, MARYPRISCA, FYANDOMO WATOA MSAADA KWA WAHANGA WA MAFURIKO WILAYANI KYELA NA BUSOKELO
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson, Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye ni Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya na Suma Ikenda Fyandomo Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya wamewatembelea kuwapa faraja na kutoa msaada wa chakula kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko Wilaya ya Kyela na Busokelo Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Akitoa taarifa Kijiji cha Kisale Kata ya Ipinda kwa viongozi hao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Ezekiel Magehema alisema baadhi ya wananchi chakula kimeharibika, nyumba zao zimeboka pia mazao yamesombwa na maji hivyo wanawakati mgumu wa kujikimu ambapo baadhi wamehifadhiwa na ndugu zao.
Wednesday, May 5, 2021
MV MBEYA II KUSITISHA SAFARI ZAKE KWA MUDA
Akizungumza na chombo kimoja habari leo Jumatano Mei 5, 2021 Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kitta amesema abiria waliokuwa katika meli hiyo walioshindwa kurejea majumbani mwao baada ya tukio hilo watarejeshewa nauli zao, watapewa chakula na maradhi.
"Meli ya Mv Mbeya II kwa sasa haitoweza kuendelea na safari mpaka itakapofanyiwa uchunguzi wa kina wa kitaalam na tukijiridhisha itaruhusiwa kuendelea na safari na baadhi ya abiria wamewezeshwa sehemu ya maradhi ya chakula mpaka watakapoanza safari ya kwenda walikokuwa wakienda,” amesema Kitta.
Amesema kikao cha kamati ya ulinzi na usalama kitafanyika kwa ajili ya kufanya tathmini ya mahitaji ya Wananchi waliokuwa safarini mpaka uchunguzi wa meli hiyo utakapokamilika na kuendelea na safari.
Aidha, amesema baadhi ya abiria walipanda mabasi baada ya kurejeshewa nauli.
Monday, May 3, 2021
UFAFANUZI WA SPIKA NDUGAI KUHUSU UBUNGE WA AKINA HALIMA MDEE NA WENZAKE
"Aandike barua aambatanishe na katiba ya chama chake, aniambatanishie na muhtasari wa hicho kikao kilichofanya hayo maamuzi, inawezekana huyo Katibu Mkuu kaamka tu kaandika halafu na mimi nakurupuka nachukua hatua, nitakua ni Spika au kitu cha ajabu, hivyo andika ili ile barua niwape watalam waangalie, halafu namuuliza msajili wa chama hawa wajumbe walioorodheshwa ndiyo wajumbe halisi?", amesema
Spika Ndugai
UJUMBE WA BALOZI WA SWEDEN TANZANIA KWA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA
![]() |
| Balozi wa Sweden Tanzania, Mh. Anders Sjöberg. |
"Mimi kama Balozi wa Sweden ninafurahi kuwepo leo kusherekea uhuru wa
habari na kujieleza. Sweden na Tanzania ni marafiki wa siku nyingi, na
wote tunatambua kwamba nguzo hii, sambamba na haki ya kupata taarifa ni
muhimu sana kwa jamii inayoheshimu Demokrasia na Haki za Binadamu"."Sweden inaamini kwamba maendeleo ya nchi yoyote ile yanapatikana kwa kupeana tarifa, kujadiliana kwa uwazi, na kuwajibishana. Basi sisi tutaendelea kuungana na watanzania wote katika jitihada za kukuza na kuendeleza uhuru wa habari na kujieleza nchini". Balozi Anders Sjöberg
Wednesday, March 17, 2021
WATAALAMU WA DAWA ZA USINGIZI WAASWA KUENDELEZA UJUZI WA ELIMU WALIYOPATA
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amewaasa watalaam wa utoaji salama wa dawa za usingizi katika shule ya dawa za usingizi iliyopo Hospitali ya Rufaa ya Kanda hiyo kuwa wanaporudi kwenye vituo vyao vya kazi kuendeleza ujuzi, elimu waliyopata pamoja na ushirikiano walioupata ili kuboresha huduma za upasuaji nchini.
Aidha Mkurugenzi huyo amewataka watalaam hao kujikita katika mbinu nyingine ya kujiongezea kipato ili kustawisha uchumi wao binafsi.









