WAWEKAZAJI WA UTALII MKOA WA TANGA WATAKIWA KUJIANDAA NA MKUTANO WA WADAU WA MAZAO YA NYUKI DUNIANI 2027.
Wadau
wa sekta ya utalii, sekta ya ufugaji nyuki na mazao yatokanayo na Nyuki
wametakiwa kujiandaa na mkutano mkubwa wa wadau wa ufugaji nyuki na
wazalishaji wa mazao yatokanayo na ufugaji nyuki utakao fanyika Jijiji
Arusha mwaka 2027.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.
Dunstan Kitandula amesema hayo alipokuwa anatoa salamu za Wizara kwenye
Kongamano la Uwekezaji, Biashara na Utalii na Uzinduzi wa Mwongozo wa
uwekezaji Mkoa wa Tanga.
Mh. Kitandula alisema kwamba kupitia
mada mbalimbali zitakazowasilishwa katika kongamano na maonesho
yanayoendelea katika mabanda, anaamini kuwa wawekezaji wengi watavutiwa
kuja kuwekeza katika Mkoa wa Tanga kwani fursa nyingi zitaelezwa hapa
zikiwemo za sekta ya Utalii.
Mh. Kitandula aliongeza kuwa mkoa
una fursa za uwekezaji kwenye malazi (Hotel na Permanent Tented Camps)
katika Hifadhi za Taifa Saadani na Mkomazi na Msitu wa Asili wa Amani
(Amani Nature Forest Reserve), fursa za uwekezaji kwenye campsites
katika mapango ya Amboni.
Pia aliongeza kuwa, kuna fursa za
uwekezaji katika usafiri na usafirishaji wa watalii kwa magari, fursa za
uwekezaji katika mashamba ya miti, uwekezaji katika viwanda vya misitu,
fursa za uwekezaji katika ufugaji nyuki na biashara ya mazao ya asali.
‘Kuna
fursa za kiuchumi kwa kuendesha biashara za aina mbalimbali (vyakula,
vinywaji na bidhaa za asili na za kitamaduni) na uwekezaji katika utalii
wa fukwe na ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Tanga unapakana na bahari ya
Hindi’ alisema Mh. Kitandula
Aidha Mh. Kitandula alimsukuru Mh.
Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye
ni Balozi wetu namba moja katika Sekta ya Utalii nchini katika kutangaza
vivutio vya Utalii pamoja na fursa za uwekezaji kupitia progamu yake ya
Tanzania - The Royal Tour ambayo inaendelea kuitangaza nchi yetu katika
masoko ya kimataifa ya utalii, pamoja na kuvutia uwekezaji katika sekta
mbalimbali za kiuchumi nchini ikiwemo Utalii.
No comments:
Post a Comment