Mh. Juma Homera, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. |
Na Keneth Mwakandyali.
Wananchi mkoani wa Mbeya wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutumia fursa
ya Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Sheria inayofanyika kitaifa mkoani
hapa kuanzia Novemba 01 hadi Novemba 12 katika viwanja vya Ruanda
Nzovwe.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera
leo Novemba alipokua akitoa akizungumza na waandishi wa Habari ambapo
amewataka wananchi kuchangamkia fursa hii ili kuweza kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili.
“Kutakuwa na timu ya wataalamu watakaokua wanazunguka maeneo mbalimbali ya wazi, vizuizini, mashuleni kutoa elimu wa msaada wa kisheria katika Nyanja tofauti kama ardhi, ndoa, mirathi, haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu kuanzia Novemba 01 mpaka Novemba 07”
“Kuna
changamoto nyingi kwenye secta hii ndio maana shughuli hii ya wiki wa
msaada wa kisheria kufanyika kitaifa mkoani Mbeya inakwenda kuleta fursa
kwa wananchi wenye changamoto mbalimbali kuweza kujua haki zao” alisema Homera
Naye mratibu wa Chama cha Sheria Tanganyika Kanda ya Mbeya
Gerinus Mzanila amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupata fursa ya kuweza
kusaidiwa changamoto za kisheria walizonazo na kujitanua katika nyanja za
kisheria.
“huduma ya msaada wa kisheria ni huduma ambayo inatolewa kwa
mtu ambae hana uwezo wa kumudu gharama za huduma ya kisheria, zile ambazo
zinatolewa mahakamani au kwa wakili. Huduma ya kisheria ipo katika nyanja nyingi
kama vile kumuhoji na kusikiliza jambo lake, kumsaidia kuandaa nyaraka
anazotakiwa kwenda kuzisajili mahakamani, usuluhishi wa amani, pia kutoa elimu
kuhusiana na mambo mbalimbali ya kisheria” amesema Mzanila
Aidha Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya Stella Kategile ameeleza kuwa
wiki ya msaada wa kisheria imekua msaada mkubwa katika jamii kwani imejikita zaidi
katika kutoa msaada kwa wananchi ambao hawana kipato na kushindwa kumudu
gharama za huduma ya kisheria.
No comments:
Post a Comment