Kampeni hiyo yenye lengo la kuhamasisha vijana kwenye vyuo vya elimu ya juu 9 na kufikia vijana 4,000 Jijini Mbeya kwa ufadhiri wa Shirika la HJMRI ambayo inaendeshwa kwa makundi mbalimbali mkoani hapa.
Saturday, December 16, 2023
KAMPENI YA 'AFYA CHECK' YAVUTIA VIJANA KUPIMA VVU KWA HIARI MKOANI MBEYA.
Kampeni hiyo yenye lengo la kuhamasisha vijana kwenye vyuo vya elimu ya juu 9 na kufikia vijana 4,000 Jijini Mbeya kwa ufadhiri wa Shirika la HJMRI ambayo inaendeshwa kwa makundi mbalimbali mkoani hapa.
Thursday, December 14, 2023
TULIA TRUST YAHITIMISHA ZOEZI LA KUPEPERUSHA BENDERA YA UPENDO.
Taasisi ya Tulia Trust jana imehitimisha zoezi la kupeperusha bendera yenye ujumbe maalum wa Upendo, Uwajibikaji kwa jamii Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya ambayo ilianza kupeperushwa Desemba 9 mwaka huu.
Ofisa Habari na Mawasiliano, Joshua Mwakanolo amesema leo wilayani humo wakati akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Makandana.
Tuesday, December 12, 2023
WANANCHI WAOMBA KUAZISHWA KWA HALMASHAURI MPYA MAKETE, NJOMBE.
Kikao cha kupata maoni ya wadau mbalimbali juu ya kupata halmashauri mpya ya wilaya ambayo wamependekeza kuipa jina la halmashauri ya wilaya kitulo ni kutokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma kutokana na umbali kutoka makao makuu ya halmashauri ya wilaya mama ya Makete.
Wananchi wameiomba selikali kuwepo na halmashauri mbili ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo vyeti ya kuzaliwa, vitambulisho vya NIDA, huduma benki na huduma nyingine za kijamii.
Mwenyekiti wa kikao hicho Bi. Rhoda Nsemwa ameiambia Mwananchi kuwa wananchi wasihofu kuhusu vigezo kwa kuwa serikali inaangalia mambo mengi hadi kufikia hatua ya kugawa eneo la kiutawala na kuwa halmashauri ya wilaya.
Monday, December 11, 2023
ZAIDI YA WATU 233,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA MUGANGO KIABAKARI, BUTIAMA
Mhandisi Mahundi ameyasema hayo Desemba 11, 2023 Wilayani Butiama Mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa maji wa Mugango Kiabakari na Mradi wa Maji wa Kijiji cha Kyankoma Kiagata.
Sunday, December 10, 2023
TULIA TRUST YAKABIDHI KITI MWENDO KWA MLEMAVU ALIYESOTA MIAKA SABA RUNGWE.
Kiti hicho kimekabidhiwa jana na Ofisa Uhusiano na Mawasiliano, Joshua Mwakanolo kwa bibi wa mlemavu huyo Justina Seme (80) kwa lengo la kumsaidia kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Pia Mwakanolo alikabidhi bendera yenye ujumbe maalum wa uwajibikaji, upendo na ushirikishwaji kwa jamii ikiwa ni maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi kitimwendo, Mwakanolo amesema kitendo hicho ni kuikumbusha jamii kurejea kwenye dhana ya uwajibikaji, upendo, mshikamano na ushirikiano.
Saturday, December 9, 2023
SAA TISA BARABARA YA MBEYA - TUNDUMA YAFUNGWA, WANANCHI WALILIA NJIA NNE.
Shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo zimekwama kwa zaidi ya saa tisa katika eneo la Simike barabara kuu ya Mbeya - Tuduma baada ya gari la mizigo kuanguka na kuziba njia.
Ajali hiyo imesababisha kuziba njia na kufanya shughuli za usafiri na usafirishaji kwenda mikoa na nchi jirani kusimama tangu saa 3:30 - hadi saa 12:00 baada gari hilo kuvutwa.
Lugano Asumwisye mkazi wa Uyole ameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa barabara ya njia nne kwani ufinyu wa barabara imekua kero na kukwamisha shughuli za kiuchumi na kupoteza mapato ya serikali.
"Ni muda sasa tunasikia ujenzi wa njia nne utaanza ila tunaona hatua zinazochukuliwa zinaenda taratibu sana, serikali iliangalie hili kwa umuhimu wake linakwamisha mambo mengi, tangu saa tatu nipo hapa ningekua nimeshafika Tunduma na kuendelea na shughuli zangu".
Serikali inakusudia kujenga barabara ya njia nne itakayosaidia kupunguza msongamano wa magari kutoka Nsalaga hadi Ifisi (Km 29) barabara itayogharimu Bilioni 138.7.
VICOBA KUWAKOMBOA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA.
Friday, December 8, 2023
MAADHIMISHO YA MIAKA 62 YA UHURU WA TANGANYIKA.
Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jaffary Haniu amewahamasisha wananchi kushiriki shughuli za usafi, upandaji miti na michezo mbalimbali sambamba na kudumisha amani na utulivu iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu.
Maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Tandale Tukuyu Mjini ambapo pamoja na mambo mengine itashuhudiwa michezo mbalimbali ikifanyika.
Kauli mbiu katika maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Umoja na mshikamano ni chachu ya maendeleo ya Taifa letu".
Wednesday, December 6, 2023
CHUTCU WACHANGIA VITANDA NA MASHUKA KITUO CHA AFYA LUPA WILAYANI CHUNYA.
Meneja Mkuu wa CHUTCU, Christian Msigwa amekabidhi msaada huo jana kwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Saimon Mayeka Saimon katika hafla fupi iliyofanyika katika Kituo hicho cha afya.
“Miongoni mwa vitu tulivyokabidhi ni pamoja na vitanda vitatu, kimoja cha kujifungulia, uchunguzi, taa maalum na mashuka 20 vyote vikiwa na thamani ya Sh 4 million” amesema Msigwa.
Tuesday, December 5, 2023
DC HANIU AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA).
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu amezindua zoezi la ugawaji wa Vitambulisho Taifa (NIDA) leo Desemba 5, 2023.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Kata ya Kyimo wilayani humo, Haniu ameeleza kuwa jumla ya vitambulisho 69638 vitatolewa kwa Wakazi wa wilaya ya Rungwe huku Kata ya Kyimo ikipokea jumla ya vitambulisho 2850.
JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAMSHUKURU IGP KWA KUWAONGEZEA VITENDEA KAZI.
Wakaguzi wa Kata nane Mkoani Mbeya wamekabidhiwa pikipiki aina ya Boxer
kwa ajili ya kurahisisha na kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu
yao katika Kata hizo.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya pikipiki hizo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Benjamin
Kuzaga amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura
kwa kutambua umuhimu wa vitendea kazi katika kufanikisha utekelezaji wa
kazi mbalimbali kwa wakaguzi wa Kata.
Saturday, December 2, 2023
WANANCHI WATAKIWA KUACHA UTAMADUNI WA KUHIFADHI MAJUMBANI MIILI YA NDUGU ZAO WALIOFARIKI.
Wananchi Wilayani Mbarali wametakiwa kuacha utamaduni wa kuhifadhi majumbani miili ya wapendwa wao waliopoteza maisha na badala yake wawapeleke katika vituo vya kutokelea huduma za afya kwani serikali imeboresha huduma za afya ikiwemo vyumba vya kuifadhia maiti.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Dkt. Ray Salandi mbele ya kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya ilipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama hicho katika sekta ya elimu na afya ukiwemo mradi wa jengo la kuhifadhi maiti ‘mochwari’ katika Hospitali ya Wilaya ya Mbarali.
Dkt. Salandi amesema serikali imenunua mashine nyingi za kuhifidhia maiti akivitaja vituo vya afya vya Madibila, Utengule Usangu na Rujewa kuwa kila kimoja kina mashine yenye uwezo wa kuhifadhi maiti tatu huku Hospital ya Wilaya ikiwa na mashine ya kuhifadhi miili kumi na mbili kwa wakati mmoja hivyo kama wilaya ina nafasi za kuhifadhi Maiti 21.
Friday, December 1, 2023
DC RUNGWE AKEMEA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO.
Mkuu
wa Wilaya ya Rungwe Jaffary Haniu amekemea vitendo vya ukatili kwa
watoto na jamii kwa ujumla ambavyo kwa namna moja au nyingine
vinachangia kuongezeka kwa maambukizi ya UKIMWI.
Akihutubia
katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo kwa Mkoa ya Mbeya
yamefanyika Wilayani Rungwe, Haniu ametaja vitendo ukatili kuwa ni
pamoja na ubakaji ulawiti na ukeketaji katika baadhi ya mikoa nchini
Tanzania.



















