Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Kanali Denis Mwela akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mara baada ya uzinduzi wa chanjo ya Surua na Rubella.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya imelazimika kutumia usafiri wa bodaboda na Powertiller kwa ajili ya kuwafikisha wataalam wa afya kwa ajili ya kutoa chanjo ya surua na rubella katika maeneo yasiyofikika.
Hatua hiyo ilitokana na na changamoto ya baadhi ya maeneo kupata athari za uharibifu wa miundombinu ikiwepo kukatika kwa mawasiliano ya barabara, vivuko, madaraja na makaravati kuharibiwa na maji ya mvua yaliyosababisha mafuriko Januari 30 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbarali, Missana Kwangura akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Mkurugenzi wa halmashauri, Missana Kwangura amewaambia waandishi habari kwamba matarajio ni kutoa chanjo kwa watoto 64,343 huku wakiwa wamepokea chanjo 74,000 ikiwepo ziada ya 5,000.

























.jpeg)