Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Serikali imetenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha matibabu ya Saratani katika Mkoa wa Mbeya.
Mwalimu amesema hayo juzi Juni 10, 2024 wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika Bunge la 12 mkutano wa 15 kikao cha 39 Bungeni Jijini Dodoma akijibu mswali la Mbunge wa Moshi vijijini Prof. Patrick Alois Ndakidemi aliyetaka kujua ni lini Serikali inampango gani kuwasaidia wagonjwa wa Saratani wasipate usumbufu wa kwenda Hospitali ya Ocen Roud kwa kuwajengea kituo na kuwawekea vifaa tiba?
“Kupitia bajeti ya Wizara ya Mwaka wa fedha 2024/25 iliyopitishwa na bunge tayari fedha imetengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho tunaamini kitanufaisha watu wa Mkoa wa Katavi, Rukwa, Njombe na Iringa” amesema Mwalimu.
Amesema uwepo wa kituo hicho utasaidia kupunguza gharama za Matibabu na kupunguza rufaa kwa wananchi wa Nyanda za juu Kusini.
Mwalimu ameongeza kuwa Kupitia bajeti ya Wizara ya Afya na TAMISEMI imetenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba ambavyo vitasambazwa katika hospitali na vituo vyote vya Afya nchi.
“Hii ni kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu katika nchi yetu kuhakikisha vifaa tiba vya kisasa vinapatikana katika ngazi ya Zahanati na vituo vyote vya Afya”.
No comments:
Post a Comment