Friday, June 7, 2024

DKT. TULIA AWAPA TABASAMU WANANCHI WA ITAGANO KWA KUCHANGIA MATENKI YA MAJI KITUO CHA AFYA

Diwani Kata ya Itagano Jijini Mbeya,Yuda Sikawenga ameungana na wananchi kuishukuru Taasisi ya Tulia Trust kwa kuchangia matenki mawili ya maji yenye ujazo wa lita 5,000 kila moja.

Taasisi hiyo ambayo Mkurugenzi wake ni  Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson ambayo inajihusisha kuwezesha wananchi kiuchumi na kuchangia miradi ya afya na elimu.

Makabidhiano ya matenki yamefanyika leo ijumaa Juni 7, 2024 kwenye kituo cha afya Itagano ikiwa ni ahadi ikitolewa na Dkt. Tulia mara baada ya kufanya ziara hivi karibuni.


Akizingumza kwa niaba ya wananchi, Yuda amesema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto ya tatizo la maji licha ya kuwepo kwa ukosefu wa chumba cha upasuaji.

Mganga Mkuu wa Jiji Dkt. Yesaya Mwasubula amesema wanamshukuru Dkt. Tulia kwa kutoa msaada huo, huku kuhusu ucheleweshaji wa kukamilisha chumba cha upasuaji amehaidi  ndani ya mwezi mmoja kitakamilika na kutoa huduma.

Ofisa habari na Mawasilino, Addy Kalinjila amesema mbali na kukabidhi msaada huo pia wameshiriki zoezi la kupanda miti ili kutunza mazingira.

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Beno Malisa, Ofisa Tarafa Kata ya Sisimba John Mboya amesema wana kila sababu kuunga mkono juhudi za Dkt. Tulia katika kuunga mkono juhudi za serikali kuchangia huduma za afya, elimu.

No comments:

Post a Comment