Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine Manase, ameagiza kamati ya maendeleo kata ya Ngana kukamilisha miradi na matumizi sahihi ya fedha.
Manase amesema hayo kwenye mkutano wa adhara wa kusikiliza kero za wananchi baada ya kupokea malalamiko ya kutosomewa mapato na matumizi, maji na ujenzi matundu ya vyoo kwenye soko na shule ya msingi Kasumuru.
"Naagiza kamati ya maendeleo kata ya Ngana kusimamia vyema fedha za miradi iliyo elekezwa na serikali sambamba na kuomba wananchi kutoa ushikiriano" amesema Manase.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri, Frola Luhala amesema atashirikiana na wananchi kutatua kero mbalimbali ikiwepo ujenzi wa choo katika soko la kasumuru na shule ya msingi.
"Tutahakikisha changamoto zinatatuliwa sambamba na tatizo la maji lengo ni kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha huduma za kijamii" amesema Luhala.
Katika mkutano huo wananchi wameishukuru serikali kwa kutatua changamoto jambo ambalo litasogeza huduma bora na kuchoche shughuli za maendeleo.

No comments:
Post a Comment