Monday, June 3, 2024

MCHECHU AIKABIDHI MBEYA - WWSA KUENDESHA KAMPUNI YA SOWACO

Msajili wa hazina, Nehemiah Mchechu ameshiriki makabidhiano ya Kampuni ya Maji Songwe (SOWACO) vikipo  mali, ardhi, mitambo kwa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya, (Mbeya - WSSA ).

Mchechu amesema hatua ya serikali kuikabidhi Mbeya - WSSA kusimamia kampuni hiyo ni baada ya kubainia kuwepo kwa changamoto mbalimbali za kiutendaji.

Amesema mali za Kampuni SOWACO zilizokabidhiwa kwa Mamlaka ya Maji Mbeya zina thamani ya  Tsh. Milioni 985 ikiwepo ardhi mitambo ambavyo vitaleta chachu ya usambazaji wa huduma kwa wananchi katika wilaya ya Mbeya hususan kwa mji wa bonde la Songwe.


Amesema lengo la serikali ni kuboresha huduma kwa wananchi sambamba na kukumbusha uwajibikaji kwa watumishi kwani serikali itangalia vigezo vya utendaji wa kazi ikiwa ni kutekeleza 4R za Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya maji Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Gilbert Kayange ameishukuru Serikali ya Rais Samia Suruhu Hassan kwa kuongeza utendaji wa mamlaka kusimamia kampuni ya 'SOWACO'.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema kitendo cha serikali kuridhia kampuni hiyo kusimamiwa na Mbeya - WSSA kutaongeza kusogeza huduma ya maji kwa wananchi.

"Nishukuru Msajili wa Hazina kwa kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi ya kimkakati Mkoa wa Mbeya." amesema Homera.

No comments:

Post a Comment