Wednesday, June 12, 2024

'NJEZA CUP' KUHAMASISHA MICHEZO NA KUIBUA VIPAJI KWA VIJANA

Mbunge wa Jimbo la Mbeya vijijini Oran Njeza, amwaga vifaa vya michezo jimboni kwake kwa lengo la kuhamasisha michezo kupitia mashindano maarufu kama "Njeza Cup" yatakayoanza hivi karibuni katika viwanja mbalimbali.

Mashindano hayo yatashirikisha timu kutoka kata zote za za Mbeya vijijini huku lengo likiwa kuhamasisha michezo kwa kulinda afya na kujenga mshikamano pamoja na mahusiano kwa vijana.

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge Njeza, Katibu wake Peter Mtepa amesema hii ni mikakati yao katika kuhakikisha wanaibua vipaji vya vijana kupitia michezo.

Mtepa amesema hayo jana Juni 11, 2024 wakati akigawa jezi kwa timu tatu kutoka Kata ya Inyala ambazo ni Timu ya Darajani FC, Imezu City FC pamoja na Mwakwenje.

Amesema michuano ya ligi ya Njeza Cup wanataraji ushiriki wa timu mbalimbali huku kukiwa na zawadi zitakazotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo ambazo kwa sasa hakuweka wazi.

Diwani wa kata ya Inyala ambae pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mwalingo Kisemba amemshukuru Mbunge Njeza kwa dhamira yake njema kuwa mdau wa michezo jimboni kwake.

No comments:

Post a Comment