Tuesday, June 11, 2024

SANAA INALIPA: KIJANA AINGIZA LAKI MOJA NDANI YA DAKIKA TANO

Kijana Lusekelo mkazi wa Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya amejipatia shilingi zaidi ya laki moja kutoka kwa Dkt. Godlove Mbwanji Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya baada ya kijana huyo kuonesha umahiri wake baada ya kuchora sura yake.

Mapatano ya awali ilikuwa ni kumchora kwa gharama ya shilingi elfu kumi na tano kama atapatia sura yake kama atakosea kidogo atampa ujira wa shilingi elfu kumi lakini baada ya kupatia vema sura yake Dkt. Mbwanji alitoa shilingi laki moja.

Aidha Dkt. Mbwanji ameahidi kumsomesha kijana huyo Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA) sanjari na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwasomesha watoto kile wanachokipenda na wananchokiweza.

"Waweza kung'angania mtoto asome masomo ya sayansi au hesabu ambayo wewe ungependa mtoto asome lakini mtoto hana uwezo nayo hivyo kujikuta anafeli unakuwa umempotezea muda" alisema Dkt. Mbwanji.

Kijana huyo ameibuka Uwanja wa Sokoine kwenye tamasha la michezo liliojumuisha wafanyakazi zaidi ya elfu moja mia mbili ikihusisha michezo mbalimbali kama soka, mpira wa pete, riadha, nyimbo, kuvuta kamba, bao, draft, pool, mavazi na maigizo ambapo washindi walipatiwa zawadi mbalimbali na vikombe.

No comments:

Post a Comment