Tuesday, June 25, 2024

CHUNYA YAPAMBANA KUKAMILISHA UWANJA KABLA YA KUANZA MSIMU MPYA WA LIGI KUU 2024/ 2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Tamim Kambona amesema Halmashauri yake imetenga shilingi milioni mia mbili kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa michezo uliopo Kata ya Mbugani unaomilikiwa na Halmashauri ili ukamilike kabla ya kuanza kwa ligi Kuu mwaka 2024/ 2025 utakaotumiwa na timu ya Ken Gold iliyopanda daraja msimu huu.

Akizungumza na MBPC blog Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya amesema mbali ya kutenga fedha hiyo kupitia mapato yake ya ndani pia imeunda kamati ya wadau inayoongozwa na Ayoub Omary.

Kambona amesema sanjari na mipango ya kamati Halmashauri inatarajia kutenga fedha nyingi zaidi mwaka ujao wa fedha ambapo uwanja huo wa kisasa utatandikwa zuria kwa ajili ya mpira wa miguu.

UKOSEFU WA BARABARA UNAVYOCHANGIA VIFO VYA WAJAWAZITO, WATOTO WACHANGA KIJIJINI IKOMBE

PICHA- Wavuvi wakiendelea kuchambua nyavu zao ndani ya mtumbwi kwenye fukwe ya Ziwa Nyasa iliyopo katika kijiji cha Ikombe, Kata ya Matema wilayani Kyela. Mitumbwi kama hii pia ndiyo hutumika kusafirishia wagonjwa na wajawazito kutoka Kijiji cha Ikombe kwenda Kituo cha Afya kilichopo Matema hatua ambayo huatarisha maisha yao hasa ziwa hilo linapokuwa na dhoruba kali.(Picha na Joachim Nyambo).

Na Joachim Nyambo.

1976 ndiyo Mwaka kilipoanzishwa Kijiji cha Ikombe kilichopo katika Kata ya Matema wilayani Kyela Mkoani Mbeya. Shughuli kubwa ya wakazi wa kijiji hiki ni uvuvi hasa wa samaki na dagaa, kilimo pamoja na ufinyanzi wa zana mbalimbali zitokanazo na udongo ikiwemo vyungu.

Wajawazito kujifungulia majumbani au wakiwa safarini ni sehemu ya changamoto zinazowakabili wakazi wa kijiji hiki kwa miaka yote waliyoishi hapa. Ni kijiji kilicho pembezoni mwa Ziwa Nyasa kikiwa kwenye safu za milima ya Livingstone.

Kukosekana kwa barabara ndiyo sababu kubwa ya wagonjwa na wajawazito kutozifikia huduma stahiki kwa wakati. Wakazi wanategemea kupata huduma za matibabu katika Kituo cha Afya kilichopo Matema yalipo makao makuu ya kata. Ni umbali wa kilometa saba kutoka kijijini hapa.

Wednesday, June 19, 2024

DC SONGWE AZUIA WACHIMBAJI WADOGO ZAIDI YA 300 KUCHIMBA MADINI

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Kitongoji cha Kampilipili Kijiji cha Mbangala Kata ya Mbangala Wilaya ya Songwe Tarafa ya Kwimba Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe wamemuomba Waziri wa Madini Anthon Mavunde na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro katika Kitalu cha Madini kinachomilikiwa na Kampuni ya Denic Mining Limited na Kikundi cha Wachimbaji cha Kampilipili Gold Mine baada ya Mkuu wa Wilaya Songwe Solomon Itunda kuzuia shughuli zote eneo la mgogoro.

Baadhi ya wachimbaji wamepaza sauti zao wakionesha masikitiko yao zaidi wakiituhumu Ofisi ya Madini Mkoa wa Songwe wakidai mchakato wa utoaji leseni umegubikwa na rushwa.

Nelson Kanunga mkazi wa Kampilipili amesema kilio chao ni kunyang’anywa eneo lao kwa dhuluma na maafisa madini kwani wamekuwepo eneo hilo yango mwaka 2011 ambapo zaidi ya watu elfu tatu wameathiriwa na mgogoro huo na kuhatarisha amani hivyo amemuomba Waziri wa Madini na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuingilia kati.

Wednesday, June 12, 2024

SERIKALI KUJENGA KITUO CHA SARATANI MBEYA

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Serikali imetenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha matibabu ya Saratani katika Mkoa wa Mbeya.

Mwalimu amesema hayo juzi Juni 10, 2024 wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika Bunge la 12 mkutano wa 15 kikao cha 39 Bungeni Jijini Dodoma akijibu mswali la Mbunge wa Moshi vijijini Prof. Patrick Alois Ndakidemi aliyetaka kujua ni lini Serikali inampango gani kuwasaidia wagonjwa wa Saratani wasipate usumbufu wa kwenda Hospitali ya Ocen Roud kwa kuwajengea kituo na kuwawekea vifaa tiba?

“Kupitia bajeti ya Wizara ya Mwaka wa fedha 2024/25 iliyopitishwa na bunge tayari fedha imetengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho tunaamini kitanufaisha watu wa Mkoa wa Katavi, Rukwa, Njombe na Iringa” amesema Mwalimu.

'NJEZA CUP' KUHAMASISHA MICHEZO NA KUIBUA VIPAJI KWA VIJANA

Mbunge wa Jimbo la Mbeya vijijini Oran Njeza, amwaga vifaa vya michezo jimboni kwake kwa lengo la kuhamasisha michezo kupitia mashindano maarufu kama "Njeza Cup" yatakayoanza hivi karibuni katika viwanja mbalimbali.

Mashindano hayo yatashirikisha timu kutoka kata zote za za Mbeya vijijini huku lengo likiwa kuhamasisha michezo kwa kulinda afya na kujenga mshikamano pamoja na mahusiano kwa vijana.

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge Njeza, Katibu wake Peter Mtepa amesema hii ni mikakati yao katika kuhakikisha wanaibua vipaji vya vijana kupitia michezo.

Mtepa amesema hayo jana Juni 11, 2024 wakati akigawa jezi kwa timu tatu kutoka Kata ya Inyala ambazo ni Timu ya Darajani FC, Imezu City FC pamoja na Mwakwenje.

Amesema michuano ya ligi ya Njeza Cup wanataraji ushiriki wa timu mbalimbali huku kukiwa na zawadi zitakazotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo ambazo kwa sasa hakuweka wazi.

Diwani wa kata ya Inyala ambae pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mwalingo Kisemba amemshukuru Mbunge Njeza kwa dhamira yake njema kuwa mdau wa michezo jimboni kwake.

Tuesday, June 11, 2024

SANAA INALIPA: KIJANA AINGIZA LAKI MOJA NDANI YA DAKIKA TANO

Kijana Lusekelo mkazi wa Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya amejipatia shilingi zaidi ya laki moja kutoka kwa Dkt. Godlove Mbwanji Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya baada ya kijana huyo kuonesha umahiri wake baada ya kuchora sura yake.

Mapatano ya awali ilikuwa ni kumchora kwa gharama ya shilingi elfu kumi na tano kama atapatia sura yake kama atakosea kidogo atampa ujira wa shilingi elfu kumi lakini baada ya kupatia vema sura yake Dkt. Mbwanji alitoa shilingi laki moja.

Aidha Dkt. Mbwanji ameahidi kumsomesha kijana huyo Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA) sanjari na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwasomesha watoto kile wanachokipenda na wananchokiweza.

"Waweza kung'angania mtoto asome masomo ya sayansi au hesabu ambayo wewe ungependa mtoto asome lakini mtoto hana uwezo nayo hivyo kujikuta anafeli unakuwa umempotezea muda" alisema Dkt. Mbwanji.

Kijana huyo ameibuka Uwanja wa Sokoine kwenye tamasha la michezo liliojumuisha wafanyakazi zaidi ya elfu moja mia mbili ikihusisha michezo mbalimbali kama soka, mpira wa pete, riadha, nyimbo, kuvuta kamba, bao, draft, pool, mavazi na maigizo ambapo washindi walipatiwa zawadi mbalimbali na vikombe.

TCRA YATOA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewajengea uwezo waandishi wa Habari Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini namna bora ya kuandika na kuzitumia vizuri kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.

Meneja wa Mawasiliano Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Boniface Shoo ameeleza kuwa mada kuu zilizowasilishwa na watumishi wa TCRA Makao makuu ni kuhusu maudhui ya mtandaoni na kanuni za utangazaji wakati uchaguzi.
 
"Duniani kote masuala ya maudhui yameshika kasi na ni muhimu kuhakikisha kwamba tunawawezesha watoa maudhui kuhusu hayo masuala ya kutoa maudhui mtandaoni ili wasitoe vitu ambavyo vinaleta uharibifu katika jamii tukielekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu" amesema Shoo.

Saturday, June 8, 2024

"AFYA NI MTAJI, TUJENGE UTAMADUNI WA KUFANYA MAZOEZI" DKT. MBWANJI

Jamii imeaswa kutumia muda wao wa ziada kufanya mazoezi ili kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kuwa na afya imara, kuongeza ushirikiano na pia kutumia michezo na vipaji kama sehemu ya kujiongezea kipato.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwaji leo Juni 08, 2024 katika kilele cha Tamasha la michezo na vipaji liliandaliwa na hospitali hiyo na kufanyika kwa wiki nzima katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

 

"Nitoe wito kwa jamii itambue mtaji mkubwa katika maisha yako ni afya yako, hivyo ni vizuri kutumia muda wa ziara tunaoupata kufanya maoezi, kama hauwezi kutenga muda maalumu wa kufanya mazoezi, basi mazoezi yawe sehemu ya mfumo wako wa maisha yako ya kila siku, kwa mfano umeenda kwenye jengo lenye ghorofa kadhaa, usitumie 'lift' kama hauna shida yeyote ya kiafya kwani hiyo itakua fursa yako ya kufanya mazoezi" amesema Dkt. Mbwanji.

Friday, June 7, 2024

DKT. TULIA AWAPA TABASAMU WANANCHI WA ITAGANO KWA KUCHANGIA MATENKI YA MAJI KITUO CHA AFYA

Diwani Kata ya Itagano Jijini Mbeya,Yuda Sikawenga ameungana na wananchi kuishukuru Taasisi ya Tulia Trust kwa kuchangia matenki mawili ya maji yenye ujazo wa lita 5,000 kila moja.

Taasisi hiyo ambayo Mkurugenzi wake ni  Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson ambayo inajihusisha kuwezesha wananchi kiuchumi na kuchangia miradi ya afya na elimu.

Makabidhiano ya matenki yamefanyika leo ijumaa Juni 7, 2024 kwenye kituo cha afya Itagano ikiwa ni ahadi ikitolewa na Dkt. Tulia mara baada ya kufanya ziara hivi karibuni.

Wednesday, June 5, 2024

AJALI YAUA WATU 13 JIJINI MBEYA



Watu 13 wamefariki Dunia leo Juni 05, 2024 baada ya Lori lililokuwa limebeba shehena ya kokoto kufeli breki na kuparamia magari mengine, bajaji na pikipiki kwenye Mteremko wa Mbembela Jijini Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 7:20 mchana katika eneo la Mbembela, Kata ya Nzonvwe Jijini Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya - Tunduma, ambapo gari lenye namba za usajili T 979 CVV na likiwa na tela namba T 758 BEU aina ya Scania iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Ross Mwaikambo (40) likitokea Shamwengo likiwa limepakia kokoto, aligongana na gari namba T 167 DLF Toyota Coaster iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika kisha kugongana na gari namba T 120 DER Toyota Harrier iliyokuwa ikiendeshwa na Dokta Robert Francis Mtungi (48) Mkazi wa Isyesye.

Kuzaga ameongeza kuwa lori hilo liligonga guta namba yenye namba za usajili MC 660 BCR iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika kisha kugonga pikipiki yenye namba MC 889 CKX iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika na kusababisha vifo vya watu kumi na tatu (13) kati yao wanawake 5, wanaume 8 na majeruhi kumi na nane (18) kati yao wanawake 4 na wanaume 14 na uharibifu wa vyombo vya moto.


Tuesday, June 4, 2024

DC KYELA ATOA MAELEKEZO USIMAMIZI WA FEDHA


Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine Manase, ameagiza kamati ya maendeleo kata ya Ngana kukamilisha miradi na matumizi sahihi ya fedha.

Manase amesema hayo kwenye mkutano wa adhara wa kusikiliza kero za wananchi baada ya kupokea malalamiko ya kutosomewa mapato na matumizi, maji na ujenzi matundu ya vyoo kwenye soko na shule ya msingi Kasumuru.

"Naagiza kamati ya maendeleo kata ya Ngana kusimamia vyema fedha za miradi iliyo elekezwa na serikali sambamba na kuomba wananchi kutoa ushikiriano" amesema Manase.

TCRA KUWASHUGHULIKIA WANAOPANDISHA BEI YA VOCHA

Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imewataka wafanyabiasha kuacha kuuza vocha zaidi ya bei elekezi kwani ni kinyume na sheria.

Monday, June 3, 2024

KAMPUNI YA PCT YAHIMIZA WAKULIMA KUZALISHA PARETO BORA

Kampuni ya Pareto Tanzania(PCT) imehamasisha wakulima kuzalisha pareto iliyobora kwa kuchuma maua yaliyokauka na ubora unaokidhi soko.

Ofisa Pareto PCT, Mussa Malubalo amesema wakati akitoa mafunzo kwa wakulima kupitia Radio ya jinsi ya kuzalisha, kupalilia na kuchuma maua ya pareto iliyo bora.

Malubalo amesema kampuni hiyo licha ya kununua pareto kwa wakulima imekuwa ikitatua changamoto ikiwepo ujenzi wa vikaushio, utoaji wa miche bora na motisha kwa kutambua mchango kwa wanaofanya vizuri.

MCHECHU AIKABIDHI MBEYA - WWSA KUENDESHA KAMPUNI YA SOWACO

Msajili wa hazina, Nehemiah Mchechu ameshiriki makabidhiano ya Kampuni ya Maji Songwe (SOWACO) vikipo  mali, ardhi, mitambo kwa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya, (Mbeya - WSSA ).

Mchechu amesema hatua ya serikali kuikabidhi Mbeya - WSSA kusimamia kampuni hiyo ni baada ya kubainia kuwepo kwa changamoto mbalimbali za kiutendaji.

Amesema mali za Kampuni SOWACO zilizokabidhiwa kwa Mamlaka ya Maji Mbeya zina thamani ya  Tsh. Milioni 985 ikiwepo ardhi mitambo ambavyo vitaleta chachu ya usambazaji wa huduma kwa wananchi katika wilaya ya Mbeya hususan kwa mji wa bonde la Songwe.

DKT. TULIA ALIPONGEZA JIJI LA MBEYA KUSHIKA NAFASI YA PILI KWA USAFI



Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amempongeza Mstahiki Meya Jiji la Mbeya, Dourmihomed Issa kwa usimamizi mzuri na kupelekea kushika nafasi ya pili kwa usafi.

Dkt. Tulia ambaye pia ni Mbunge Jimbo la Mbeya mjini amesema hayo Juni Mosi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani yaliyofanyika katika viwanja vya stendi ya Kabwe Jijini hapa.

"Leo ni siku la Mazingira duniani na sisi tumeadhimisha kwa kufanya usafi nimpongeze jiji letu la Mbeya  chini ya Mstahiki Meya Dourmohamed Issa kwa usimamizi mzuri na kuwezesha kushika nafasi ya pili katika usafi" amesema Dkt. Tulia.

Aidha amesisitiza suala la usafi kwa wananchi Mkoa wa Mbeya iwe ajenda ya kudumu katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya Jiji la Mbeya Dourmohamed Issa amesema watandelea kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na suala la usafi ili jiji liweze kupanda na kushika nafasi ya kwanza.