Monday, April 1, 2024

MWALIMU NA MWANAFUNZI WAUAWA CHUNYA

Na Ezekiel Kamanga.

Watu wawili wakazi wa Kiwanja Kata ya Mbugani Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya wanadaiwa kuuawa na mtoto mwingine mwenye umri wa miaka sita kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali nyumbani kwao.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa aliyeuawa ni mwalimu Herieth Lupembe wa shule ya msingi Mbugani aliyefahamika kwa jina la Herieth Lupembe mwingine ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela aliyekuwa anaishi naye.

Taarifa za mauaji hayo zilipatikana jioni machi 30, 2024 baada ya mwalimu huyo kutofungua duka lake na simu yake kutopatikana pia kutoonekana kanisani wakati si kawaida yake.

Baadhi ya mashuda wamedai kuwa aliagiza bidhaa za dukani kutoka Mbeya baada ya kutoonekana bidhaa hizo ziliachwa nje.

Taarifa zilitolewa kijijini kwa mwenyekiti Gideon Kinyamagiha ambapo uongozi ulitoa taarifa Polisi ambao nao walifika na kufanya uchunguzi wa awali kisha kuchukua miili na kwenda kuihifadhi Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa uchunguzi zaidi ambapo majeruhi amekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga kuthibitisha chanzo cha tukio hilo la kinyama.

No comments:

Post a Comment